Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 8:20-32

Kutoka 8:20-32 NEN

Kisha BWANA akamwambia Mose, “Amka mapema asubuhi na usimame mbele ya Farao wakati anapokwenda mtoni nawe umwambie, ‘Hili ndilo BWANA asemalo: Waachie watu wangu waende, ili wapate kuniabudu. Kama hutawaachia watu wangu waondoke nitakupelekea makundi ya mainzi juu yako, kwa maafisa wako, kwa watu wako na kwenye nyumba zenu. Nyumba za Wamisri zitajazwa mainzi, hata na ardhi yote ya Misri. “ ‘Lakini siku ile nitafanya kitu tofauti katika nchi ya Gosheni, ambapo watu wangu wanaishi, hapatakuwepo na makundi ya mainzi, ili mpate kujua kwamba Mimi, BWANA, niko katika nchi hii. Nitaweka tofauti kati ya watu wangu na watu wenu. Ishara hii ya ajabu itatokea kesho.’ ” Naye BWANA akafanya hivyo. Makundi makubwa ya mainzi yalimiminika katika jumba la kifalme la Farao na katika nyumba za maafisa wake, pia nchi yote ya Misri ikaharibiwa na mainzi. Ndipo Farao akamwita Mose na Aroni na kuwaambia, “Nendeni mkamtolee Mungu wenu dhabihu katika nchi hii.” Lakini Mose akamwambia, “Hilo halitakuwa sawa. Dhabihu tutakazomtolea BWANA Mungu wetu zitakuwa chukizo kwa Wamisri. Kama tukitoa dhabihu ambazo ni chukizo mbele yao, je, hawatatupiga mawe? Ni lazima twende mwendo wa siku tatu mpaka tufike jangwani ili tumtolee BWANA Mungu wetu dhabihu, kama alivyotuagiza.” Farao akamwambia, “Nitawaruhusu mwende kumtolea BWANA Mungu wenu dhabihu huko jangwani, lakini hamna ruhusa kwenda mbali sana. Sasa mniombee.” Mose akajibu, “Mara tu nitakapoondoka, nitamwomba BWANA na kesho mainzi yataondoka kwa Farao, kwa maafisa wake na kwa watu wake. Hakikisha tu kwamba Farao hatatenda kwa udanganyifu tena kwa kutokuwaachia watu waende kumtolea BWANA dhabihu.” Ndipo Mose akamwacha Farao na kumwomba BWANA, naye BWANA akafanya lile Mose alilomwomba. Mainzi yakaondoka kwa Farao, kwa maafisa wake na kwa watu wake, wala hakuna hata inzi aliyebakia. Lakini wakati huu pia Farao akaushupaza moyo wake, wala hakuwaruhusu Waisraeli waondoke.