Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 21:22-34

Mwanzo 21:22-34 NEN

Wakati huo Abimeleki na Fikoli mkuu wa majeshi yake wakamwambia Abrahamu, “Mungu yu pamoja nawe katika kila kitu unachofanya. Sasa niapie hapa mbele za Mungu kwamba hutanitenda hila mimi, watoto wangu wala wazao wangu. Nitendee mimi na nchi ambayo unaishi kama mgeni wema ule ule ambao nimekutendea.” Abrahamu akasema, “Ninaapa hivyo.” Ndipo Abrahamu akalalamika kwa Abimeleki kuhusu kisima cha maji ambacho watumishi wa Abimeleki walikuwa wamekinyangʼanya. Lakini Abimeleki akasema, “Sijui ni nani ambaye amefanya hili. Hukuniambia, leo tu ndipo ninasikia habari zake.” Hivyo Abrahamu akaleta kondoo na ngʼombe, akampa Abimeleki, nao watu hawa wawili wakafanya mapatano. Abrahamu akatenga kondoo wa kike saba kutoka kwenye kundi, Abimeleki akamuuliza Abrahamu, “Ni nini maana ya hawa kondoo wa kike saba uliowatenga peke yao?” Abrahamu akamjibu, “Upokee hawa kondoo wa kike saba kutoka mkononi mwangu kama ushahidi kuwa nilichimba kisima hiki.” Hivyo mahali pale pakaitwa Beer-Sheba, kwa sababu watu wawili waliapiana hapo. Baada ya mapatano kufanyika huko Beer-Sheba, Abimeleki na Fikoli mkuu wa majeshi yake wakarudi katika nchi ya Wafilisti. Abrahamu akapanda mti wa mkwaju huko Beer-Sheba, na hapo akaliitia jina la BWANA, Mungu wa milele. Naye Abrahamu akakaa katika nchi ya Wafilisti kwa muda mrefu.