Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 21:22-34

Mwanzo 21:22-34 SRUV

Ikawa wakati ule Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakamwambia Abrahamu, wakinena, Mungu yu pamoja nawe katika yote unayotenda. Basi sasa uniapie kwa Mungu, ya kuwa hutanitenda hila, wala mwanangu, wala mjukuu wangu, lakini kwa kadiri ya fadhili niliyokutendea utanitendea mimi, na nchi hii ambayo umetembea ndani yake. Abrahamu akasema, Nitaapa. Kisha Abrahamu akamlaumu Abimeleki kwa sababu ya kisima cha maji ambacho watumishi wa Abimeleki wamemnyang'anya. Abimeleki akasema, Mimi sijui ni nani aliyetenda neno hili, wala hukuniambia, wala sikusikia habari hii ila leo tu. Abrahamu akatwaa kondoo na ng'ombe akampa Abimeleki, na hao wawili wakafanya mapatano. Abrahamu akawaweka wana-kondoo saba wa kike peke yao. Abimeleki akamwuliza Abrahamu, Hawa wana-kondoo saba majike, uliowaweka, maana yake ni nini? Akasema, Hawa wana-kondoo saba majike utawapokea mkononi mwangu, wawe ushuhuda ya kuwa ni mimi niliyekichimba kisima hiki. Kwa hiyo akapaita mahali pale Beer-sheba, kwa sababu waliapa huko wote wawili. Basi wakafanya mapatano huko Beer-sheba. Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakaondoka wakarudi hata nchi ya Wafilisti. Abrahamu akapanda mkwaju huko Beer-sheba, akaliitia huko jina la BWANA Mungu wa milele. Abrahamu akaishi kama mgeni kwa Wafilisti siku nyingi.

Soma Mwanzo 21