Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 5:18-32

Mwanzo 5:18-32 NENO

Yaredi alipokuwa ameishi miaka mia moja na sitini na mbili (162), akamzaa Idrisi. Baada ya kumzaa Idrisi, Yaredi aliishi miaka mia nane, naye akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. Yaredi aliishi jumla ya miaka mia tisa na sitini na mbili (962), ndipo akafa. Idrisi alipokuwa ameishi miaka sitini na tano, akamzaa Methusela. Baada ya kumzaa Methusela, Idrisi alitembea na Mungu miaka mia tatu, na akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. Idrisi aliishi jumla ya miaka mia tatu sitini na tano (365). Idrisi akatembea na Mungu, kisha akatoweka, kwa sababu Mungu alimchukua. Methusela alipokuwa ameishi miaka mia moja na themanini na saba (187), akamzaa Lameki. Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka mia saba na themanini na mbili (782), akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. Methusela aliishi jumla ya miaka mia tisa sitini na tisa (969), ndipo akafa. Lameki alipokuwa ameishi miaka mia moja na themanini na mbili (182), alimzaa mwana. Akamwita jina Nuhu. Naye akasema, “Huyu ndiye atakayetufariji katika kazi ngumu ya mikono yetu yenye maumivu makali yaliyosababishwa na ardhi iliyolaaniwa na Mwenyezi Mungu.” Baada ya Nuhu kuzaliwa, Lameki aliishi miaka mia tano na tisini na tano (595), akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. Lameki aliishi jumla ya miaka mia saba sabini na saba (777), ndipo akafa. Baada ya Nuhu kuishi miaka mia tano, aliwazaa Shemu, Hamu, na Yafethi.