Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya Utangulizi

Utangulizi
Jina Isaya maana yake ni “Mwenyezi Mungu anaokoa”. Kufuatana na mapokeo, Isaya alitoa unabii wakati mmoja na Amosi, Hosea na Mika. Isaya alianza huduma yake mnamo 740 K.K. Isaya alikuwa ameoa, na akapata watoto wawili, Shear-Yashubu na Maher-Shalal-Hash-Bazi. Yamkini, Isaya alitumia wakati wake mwingi huko Yerusalemu wakati wa Mfalme Hezekia. Kufuatana na historia ya Kiyahudi, Isaya aliuawa kwa kupasuliwa vipande viwili chini ya utawala wa Manase, yule mwana mwovu wa Mfalme Hezekia, aliyetawala mnamo 696–642 K.K.
Mwandishi
Isaya mwana wa Amozi.
Kusudi
Isaya anatoa wito kwa taifa la Yuda kumrudia Mwenyezi Mungu, na pia anawatangazia wokovu wa Mwenyezi Mungu kupitia kwa Masihi.
Mahali
Yerusalemu.
Tarehe
Mnamo 700–680 K.K.
Wahusika Wakuu
Isaya, wanawe wawili Shear-Yashubu na Maher-Shalal-Hash-Bazi, Mfalme Hezekia, na watu wa Yerusalemu na Yuda.
Wazo Kuu
Kuufanya ujumbe wa Mwenyezi Mungu uwe wazi kwa Israeli, ili kuwaonya kuhusu hukumu ikiwa wataendelea kudumu katika dhambi. Pia kudhihirisha jinsi Mwenyezi Mungu atakavyoshughulika nao katika kuwarejesha chini ya Masihi wao milele.
Mambo Muhimu
Mwenyezi Mungu atamtuma Masihi ili kuokoa watu wake; atakuja kama Mwokozi na Bwana pekee, lakini atatenda kama mtumishi. Atakufa ili kuziondoa dhambi. Mwenyezi Mungu anaahidi kutuma faraja, ukombozi na urejesho katika ufalme wake ujao. Masihi atawatawala wafuasi wake wakati huo. Tumaini ni hakika kwa sababu Al-Masihi yuaja.
Yaliyomo
Hukumu na matumaini ya kurejeshwa (1:1–6:13)
Ishara mbalimbali kwa Israeli, ahadi ya kurejeshwa (7:1–12:6)
Unabii dhidi ya mataifa (13:1–23:18)
Hukumu ya Israeli na ukombozi (24:1–27:13)
Maonyo, na Sayuni kutengenezwa (28:1–35:10)
Mfalme Hezekia, Ashuru na Babeli (36:1–39:8)
Ahadi za ukombozi wa Mwenyezi Mungu (40:1–56:8)
Ukombozi, faraja na utukufu wa wakati ujao (56:9–66:24).

Iliyochaguliwa sasa

Isaya Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia