Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Wimbo 8

8
1Laiti ungekuwa kwangu kama ndugu wa kiume,
ambaye aliyanyonya matiti ya mama yangu!
Kisha, kama ningekukuta huko nje,
ningekubusu,
wala hakuna mtu yeyote angenidharau.
2Ningekuongoza na kukuleta
katika nyumba ya mama yangu,
yeye ambaye amenifundisha.
Ningekupa divai iliyokolezwa unywe,
asali ya maua ya mikomamanga yangu.
3Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu,
na mkono wake wa kuume unanikumbatia.
4Binti za Yerusalemu, ninawaagiza:
msichochee wala kuamsha mapenzi
hata yatakapotaka yenyewe.
Rafiki
5Ni nani huyu anayekuja kutoka nyikani
akimwegemea mpenzi wake?
Mpendwa
Nilikuamsha chini ya mtofaa,
huko mama yako alipotunga mimba yako,
huko yeye alipata uchungu akakuzaa.
6Nitie kama muhuri moyoni mwako,
kama muhuri kwenye mkono wako;
kwa maana upendo una nguvu kama mauti,
wivu wake ni mkatili kama Kuzimu#8:6 Kuzimu kwa Kiebrania ni Sheol, yaani Shimo lisilo na mwisho..
Unachoma kama mwali wa moto,
kama mwali mkubwa wa moto wa Mwenyezi Mungu hasa.
7Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo,
mito haiwezi kuugharikisha.
Kama mtu angetoa mali yote ya nyumbani mwake
kwa ajili ya upendo,
angedharauliwa kabisa.
Rafiki
8Tunaye dada mdogo,
matiti yake hayajakua bado.
Tutafanya nini kwa ajili ya dada yetu
wakati atakapokuja kuposwa?
9Kama yeye ni ukuta,
tutajenga minara ya fedha juu yake.
Na kama yeye ni mlango,
tutamzungushia mbao za mwerezi.
Mpendwa
10Mimi ni ukuta,
nayo matiti yangu ni kama minara.
Ndivyo ambavyo nimekuwa machoni pake
kama yule anayeleta utoshelevu.
11Sulemani alikuwa na shamba la mizabibu huko Baal-Hamoni;
alikodisha shamba lake la mizabibu kwa wapangaji.
Kila mmoja angeleta kwa ajili ya matunda yake
shekeli elfu moja#8:11 Shekeli 1,000 ni kama kilo 11.5. za fedha.
12Lakini shamba langu la mizabibu
ambalo ni langu mwenyewe
ni langu kutoa;
hizo shekeli elfu moja ni kwa ajili yako, ee Sulemani,
na shekeli mia mbili#8:12 Shekeli 200 ni kama kilo 2.3. ni kwa ajili
ya wale wanaotunza matunda yake.
Mpenzi
13Wewe ukaaye bustanini
pamoja na rafiki mliohudhuria,
hebu nisikie sauti yako!
Mpendwa
14Njoo, mpenzi wangu,
uwe kama paa
au kama ayala mchanga
juu ya milima iliyojaa manukato.

Iliyochaguliwa sasa

Wimbo 8: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia