Yakobo Utangulizi
Utangulizi
Waraka wa Yakobo unaweza kuwa mojawapo ya nyaraka za kwanza kabisa katika Injili. Inawezekana uliandikwa wakati moja na ule wa Paulo kwa Wagalatia. Waraka huu uliandikiwa wafuasi wa Al-Masihi wa Kiyahudi waliotawanyika huko Ponto, Galatia, Kapadokia, jimbo la Asia, na Bithinia ili kuwapa mawaidha kuhusu ilivyowapasa kuishi kama waumini, wakidhihirishwa na matendo mema na imani itendayo kazi. Barua hii ina mithali nyingi fupi fupi zinazosaidia kuweka wazi yale Mafundisho ya Mlimani ya Bwana Isa.
Matatizo yanayozungumziwa yalikuwa yakiwasumbua waumini. Tunasoma kuhusu kiburi, ubaguzi, choyo, tamaa, unafiki, kupenda anasa, na kusengenya. Yakobo aliandika kusahihisha makosa haya kwa kuonesha kwamba imani pasipo matendo imekufa. Hii ina maana kuwa, kusema tu kwamba unaamini hakutoshi, bali imani halisi huambatana na matendo.
Mwandishi
Yakobo, ndugu yake Isa.
Kusudi
Kuwahimiza waumini kufanya mabadiliko yanayohitajika katika maisha ya mfuasi wa Al-Masihi.
Mahali
Yerusalemu.
Tarehe
Mnamo 49 B.K.
Wahusika Wakuu
Yakobo, na Wayahudi waliotawanyika sehemu mbalimbali.
Wazo Kuu
Yakobo anasisitiza umuhimu wa mfuasi wa Al-Masihi kuishi maisha yanayodhihirisha hali yake ya ndani. Hapo ndipo ulimwengu utapata kujua jinsi Injili inavyoweza kubadili maisha ya watu.
Mambo Muhimu
Imani pasipo matendo imekufa; ili kuitimiza sheria ya upendo lazima imani yetu iwe na matendo. Yakobo anawafundisha wafuasi wa Al-Masihi kutokubaliana na hali ya kidunia kuhusu mali na utajiri. Wafuasi wa Al-Masihi wanatakiwa kujiwekea hazina kwa Mwenyezi Mungu; hivyo wafuasi wa Al-Masihi hawapaswi kuwapendelea wenye mali, wala kuwadharau maskini. Pia waombe hekima kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Yaliyomo
Salamu, na maisha ya imani ya kweli (1:1-27)
Upendeleo, imani ya kweli na matendo (2:1-26)
Kuutawala ulimi (3:1-18)
Mwenendo upasao (4:1-17)
Mawaidha ya mwisho (5:1-20).
Iliyochaguliwa sasa
Yakobo Utangulizi: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
![None](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2F58%2Fhttps%3A%2F%2Fweb-assets.youversion.com%2Fapp-icons%2Fsw.png&w=128&q=75)
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.