Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayubu 24:1-12

Ayubu 24:1-12 NEN

“Kwa nini Mwenyezi asiweke nyakati kwa ajili ya hukumu? Kwa nini wale wamjuao wazitafute siku kama hizo bila mafanikio? Watu husogeza mawe ya mpaka; huchunga makundi ya wanyama waliyonyangʼanya kwa nguvu. Huwanyangʼanya yatima punda wao, na kumchukua rehani fahali wa mjane. Humsukuma mhitaji kutoka njia, na kuwafanya maskini wote wa nchi kulazimika kujificha. Kama punda-mwitu jangwani, maskini huzunguka katika kazi zao za kutafuta chakula; mahali palipo jangwa huwapa chakula cha watoto wao. Hukusanya chakula mashambani na kuokota masazo katika mashamba ya mizabibu ya waovu. Kwa kukosa nguo, usiku kucha hukaa uchi; hawana chochote cha kujifunika baridi. Hutota kwa mvua za mlimani, nao huikumbatia miamba kwa ajili ya kukosa pa kujisitiri. Mtoto yatima hupokonywa matitini; mtoto wachanga wa maskini hunyakuliwa kwa ajili ya deni. Kwa kukosa nguo, hutembea uchi; hubeba miganda ya ngano, lakini huwa na njaa. Hukamua zeituni katika mawe ya kusagia; hukanyaga mashinikizo, lakini wanaona kiu. Kilio cha huzuni cha wanaokufa kinapaa kutoka mjini, nazo nafsi za waliojeruhiwa zinalilia msaada. Lakini Mungu hamlaumu mtu yeyote kwa kutenda mabaya.