Ayubu 34:31-37
Ayubu 34:31-37 NEN
“Kama mwanadamu akimwambia Mungu, ‘Nimekosa lakini sitatenda dhambi tena. Nifundishe nisichoweza kuona; kama nimekukosea, sitafanya hivyo tena.’ Je basi, Mungu atakulipa kwa masharti yako, wakati wewe umekataa kutubu? Yakupasa wewe uamue, wala si mimi; sasa niambie lile ulijualo. “Wanadamu wenye ufahamu husema, wenye hekima wanaonisikia huniambia, ‘Ayubu huongea bila maarifa; maneno yake hayana busara.’ Laiti Ayubu angejaribiwa hadi kikomo cha mwisho, kwa sababu anajibu kama mtu mwovu! Kwenye dhambi yake huongeza uasi; kwa dharau hupiga makofi miongoni mwetu, na kuzidisha maneno yake dhidi ya Mungu.”