Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayubu 41:1-11

Ayubu 41:1-11 NEN

“Je, waweza kumvua Lewiathani kwa ndoano ya samaki, au kufunga ulimi wake kwa kamba? Waweza kupitisha kamba puani mwake, au kutoboa taya lake kwa kulabu? Je, ataendelea kukuomba umhurumie? Atasema nawe maneno ya upole? Je, atafanya agano nawe ili umtwae awe mtumishi wako maisha yake yote? Je, utamfuga na kumfanya rafiki kama ndege, au kumfunga kamba kwa ajili ya wasichana wako? Je, wafanyabiashara watabadilishana bidhaa kwa ajili yake? Watamgawanya miongoni mwa wafanyao biashara? Je, waweza kuijaza ngozi yake kwa vyuma vyenye ncha kali, au kichwa chake kwa mkuki wa kuvulia samaki? Kama ukiweka mkono wako juu yake, utavikumbuka hivyo vita na kamwe hutarudia tena! Tumaini lolote la kumtiisha ni kujidanganya; kule kumwona tu kunamwangusha mtu chini. Hakuna yeyote aliye mkali athubutuye kumchokoza. Ni nani basi awezaye kusimama dhidi yangu? Ni nani mwenye madai dhidi yangu ili nipate kumlipa? Kila kitu kilicho chini ya mbingu ni mali yangu.