Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayubu 8

8
Bildadi anasema: Yampasa Ayubu atubu
1Kisha Bildadi Mshuhi akajibu:
2“Hata lini wewe utasema mambo kama haya?
Maneno yako ni kama upepo mkuu.
3Je, Mungu hupotosha hukumu?
Je, Mwenyezi hupotosha kile kilicho haki?
4Watoto wako walipomtenda dhambi,
aliwapa adhabu ya dhambi yao.
5Lakini ukimtafuta Mungu,
nawe ukamsihi Mwenyezi,
6ikiwa wewe ni safi na mnyofu,
hata sasa atainuka mwenyewe kwa niaba yako,
na kukurudisha katika mahali pako pa haki.
7Ijapokuwa mwanzo wako ulikuwa mdogo,
lakini mwisho wako utakuwa wa mafanikio.
8“Ukaulize vizazi vilivyotangulia
na uone baba zao walijifunza nini,
9kwa kuwa sisi tumezaliwa jana tu na hatujui lolote,
nazo siku zetu duniani ni kama kivuli tu.
10Je, hawatakufundisha na kukueleza?
Je, hawataleta maneno ya ufahamu wao?
11Je, mafunjo yaweza kumea mahali pasipo na matope?
Matete yaweza kustawi bila maji?
12Wakati bado yanaendelea kukua kabla ya kukatwa,
hunyauka haraka kuliko majani mengine.
13Huu ndio mwisho wa watu wote wanaomsahau Mungu;
vivyo hivyo matumaini ya wasiomjali Mungu huangamia.
14Lile analolitumainia huvunjika upesi;
lile analolitegemea ni utando wa buibui.
15Huutegemea utando wake, lakini hausimami;
huung’ang’ania, lakini haudumu.
16Yeye ni kama mti ulionyeshewa vizuri wakati wa jua,
ukieneza machipukizi yake bustanini;
17huifunganisha mizizi yake kwenye lundo la mawe,
na kutafuta nafasi kati ya mawe.
18Unapong’olewa kutoka mahali pake,
ndipo mahali pale huukana na kusema,
‘Mimi kamwe sikukuona.’
19Hakika uhai wake hunyauka,
na kutoka udongoni mimea mingine huota.
20“Hakika Mungu hamkatai mtu asiye na hatia,
wala kuitia nguvu mikono ya mtenda maovu.
21Bado atakijaza kinywa chako na kicheko,
na midomo yako na kelele za shangwe.
22Adui zako watavikwa aibu,
nayo mahema ya waovu hayatakuwepo tena.”

Iliyochaguliwa sasa

Ayubu 8: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia