Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yoshua 15

15
Mgawo kwa Yuda
1Mgawo kwa kabila la Yuda, ulienea kufuatana na koo zao, ukishuka kufikia eneo la Edomu, hadi Jangwa la Sini mwisho kabisa upande wa kusini.
2Mpaka wao wa kusini ulianzia ghuba iliyo kwenye ncha ya kusini mwa Bahari ya Chumvi, 3ukakatiza kusini mwa Akrabimu, ukaendelea hadi Sini, kisha ukaenda hadi kusini mwa Kadesh-Barnea. Tena ukapitia Hesroni, ukapanda hadi Adari, na ukapinda hadi Karka. 4Kisha ukaendelea hadi Azmoni, na kuunganika na Kijito cha Misri, na kuishia baharini. Huu ndio mpaka wao wa upande wa kusini.
5Mpaka wa upande wa mashariki ni Bahari ya Chumvi ukienea mahali Mto Yordani unapoingilia.
Mpaka wa upande wa kaskazini ulianzia ghuba ya bahari mahali Mto Yordani unapoingilia, 6ukapanda hadi Beth-Hogla, na kuendelea kaskazini mwa Beth-Araba hadi kwenye Jiwe la Bohani mwana wa Reubeni. 7Kisha mpaka ulipanda hadi Debiri kutoka Bonde la Akori, na kugeuka kaskazini hadi Gilgali inayotazamana na miteremko ya Adumimu, kusini mwa bonde. Ukaendelea sambamba hadi maji ya En-Shemeshi na kutokeza huko En-Rogeli. 8Kisha ukapanda kwa kufuata Bonde la Ben-Hinomu sambamba na mteremko wa kusini wa mji mkubwa wa Wayebusi (yaani Yerusalemu). Kutoka hapo ukapanda juu ya kilima magharibi mwa Bonde la Hinomu mwisho wa ncha ya kaskazini mwa Bonde la Warefai. 9Kutoka juu ya kilima, mpaka ule ukaendelea hadi kwenye chemchemi ya maji ya Neftoa, ukatokea kwenye miji ya Mlima Efroni na kuteremka kuelekea Baala (yaani Kiriath-Yearimu). 10Kisha ukapinda upande wa magharibi kutoka Baala hadi Mlima Seiri, ukafuatia sambamba mteremko wa kaskazini mwa Mlima Yearimu (yaani Kesaloni), ukashuka hadi Beth-Shemeshi, na kukatiza hadi Timna. 11Ukaelekea hadi mteremko wa kaskazini mwa Ekroni, ukageuka kuelekea Shikeroni, ukapita hadi Mlima Baala na kufika Yabineeli. Mpaka ule ukaishia baharini.
12Mpaka wa magharibi ni pwani ya Bahari Kuu.
Hii ndiyo mipaka ya watu wa Yuda kwa koo zao.
Nchi aliyopewa Kalebu
(Waamuzi 1:11-15)
13Kwa kufuata maagizo ya Mwenyezi Mungu kwake, Yoshua alimpa Kalebu mwana wa Yefune sehemu katika Yuda: Kiriath-Arba, yaani Hebroni. (Arba alikuwa baba wa zamani wa Anaki.) 14Kutoka Hebroni, Kalebu alifukuza hao Waanaki watatu: Sheshai, Ahimani na Talmai, wana wa Anaki. 15Kutoka hapo akaondoka kupigana dhidi ya watu walioishi Debiri (mji wa Debiri hapo uliitwa Kiriath-Seferi). 16Kalebu akasema, “Nitamwoza binti yangu Aksa kwa mtu atakayeweza kupigana na kuteka Kiriath-Seferi.” 17Basi Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu yake Kalebu, akauteka; hivyo Kalebu akamtoa Aksa binti yake, akaolewa naye.
18Siku moja Aksa alipokuja kwa Othnieli, alimsihi Othnieli amwombe baba yake, Kalebu, shamba. Aksa aliposhuka kutoka punda wake, Kalebu akamuuliza, “Je, wataka nikufanyie nini?”
19Akamjibu, “Naomba unifanyie jambo moja la hisani. Kwa kuwa umenipa ardhi huko Negebu, nipe pia chemchemi za maji.” Basi Kalebu akampa chemchemi za juu na za chini.
Miji ya Yuda
20Huu ndio urithi wa kabila la Yuda, kufuatana na koo zao:
21Miji ya kusini kabisa ya kabila la Yuda katika Negebu kuelekea mpaka wa Edomu ilikuwa:
Kabseeli, Ederi, Yaguri, 22Kina, Dimona, Adada, 23Kedeshi, Hazori, Ithnani, 24Zifu, Telemu, Bealothi, 25Hazor-Hadata, Kerioth-Hezroni (yaani Hazori), 26Amamu, Shema, Molada, 27Hasar-Gada, Heshmoni, Beth-Peleti, 28Hasar-Shuali, Beer-Sheba, Biziothia, 29Baala, Iyimu, Esemu, 30Eltoladi, Kesili, Horma, 31Siklagi, Madmana, Sansana, 32Lebaothi, Shilhimu, Aini na Rimoni; hiyo yote ni miji ishirini na tisa, pamoja na vijiji vyake.
33Katika Shefela#15:33 au upande wa magharibi chini ya vilima:
Eshtaoli, Sora, Ashna, 34Zanoa, En-Ganimu, Tapua, Enamu, 35Yarmuthi, Adulamu, Soko, Azeka, 36Shaaraimu, Adithaimu na Gedera (au Gederothaimu); yote ni miji kumi na nne, pamoja na vijiji vyake.
37Senani, Hadasha, Migdal-Gadi, 38Dileani, Mispa, Yoktheeli, 39Lakishi, Boskathi, Egloni, 40Kaboni, Lamasi, Kitlishi, 41Gederothi, Beth-Dagoni, Naama na Makeda; yote ni miji kumi na sita pamoja na vijiji vyake.
42Libna, Etheri, Ashani, 43Yifta, Ashna, Nesibu, 44Keila, Akzibu na Maresha; yote ni miji tisa pamoja na vijiji vyake.
45Ekroni, pamoja na makazi yake na vijiji vyake; 46magharibi mwa Ekroni, maeneo yote yaliyokuwa karibu na Ashdodi, pamoja na vijiji vyake; 47Ashdodi, makazi yake na vijiji vyake, na Gaza, makazi yake na vijiji vyake, hadi kufikia Kijito cha Misri na Pwani ya Bahari Kuu.
48Katika nchi ya vilima:
Shamiri, Yatiri, Soko, 49Dana, Kiriath-Sana (yaani Debiri), 50Anabu, Eshtemoa, Animu, 51Gosheni, Holoni na Gilo; miji kumi na moja pamoja na vijiji vyake.
52Arabu, Duma, Ashani, 53Yanimu, Beth-Tapua, Afeka, 54Humta, Kiriath-Arba (yaani Hebroni), na Siori; miji tisa pamoja na vijiji vyake.
55Maoni, Karmeli, Zifu, Yuta, 56Yezreeli, Yokdeamu, Zanoa, 57Kaini, Gibea na Timna; miji kumi pamoja na vijiji vyake.
58Halhuli, Beth-Suri, Gedori, 59Maarathi, Beth-Anothi na Eltekoni; miji sita pamoja na vijiji vyake.
60Kiriath-Baali (yaani Kiriath-Yearimu) na Raba; miji miwili pamoja na vijiji vyake.
61Huko jangwani:
Beth-Araba, Midini, Sekaka, 62Nibshani, Mji wa Chumvi, na En-Gedi; miji sita pamoja na vijiji vyake.
63Yuda hakuweza kuwafukuza Wayebusi, walioishi Yerusalemu; hadi leo Wayebusi huishi huko pamoja na watu wa Yuda.

Iliyochaguliwa sasa

Yoshua 15: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia