Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yoshua 16

16
Mgawo kwa Efraimu na Manase
1Mgawanyo wa Yusufu ulianzia Yordani ya Yeriko, mashariki mwa miji ya Yeriko na kutoka hapo ulipanda kupitia jangwani na kuingia katika nchi ya vilima ya Betheli. 2Ukaendelea kutoka Betheli (ndiyo Luzu), ukavuka kuingia eneo la Waarki huko Atarothi, 3ukateremkia kuelekea magharibi hadi eneo la Wayafleti ukienea hadi eneo la Beth-Horoni ya Chini hadi Gezeri, ukiishia baharini.
4Kwa hiyo Manase na Efraimu, wazao wa Yusufu, walipokea urithi wao.
5Hili ndilo lilikuwa eneo la Efraimu, kufuatana na koo zao:
Mpaka wa urithi wao ulianzia Ataroth-Adari upande wa mashariki hadi Beth-Horoni ya Juu, 6na kuendelea mpaka baharini. Kutoka Mikmeta upande wa kaskazini ulipinda kuelekea mashariki hadi Taanath-Shilo, ukiupita hadi Yanoa upande wa mashariki. 7Kisha uliteremka kutoka Yanoa hadi Atarothi na Naara, ukagusa Yeriko na kutokea katika Mto Yordani. 8Kutoka Tapua, mpaka ulienda magharibi hadi Bonde la Kana na kuishia baharini. Huu ulikuwa ndio urithi wa kabila la Waefraimu, kufuatana na koo zao.
9Pia ulijumuisha miji yote na vijiji vyake ambavyo vilitengwa kwa ajili ya Waefraimu ndani ya urithi wa kabila la Manase.
10Hawakuwatoa Wakanaani walioishi Gezeri; hadi leo Wakanaani wanaishi miongoni mwa watu wa Efraimu, lakini wanatumikishwa kwa kazi ngumu.

Iliyochaguliwa sasa

Yoshua 16: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia