Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maombolezo 3:1-20

Maombolezo 3:1-20 NEN

Mimi ndiye mtu aliyeona mateso kwa fimbo ya ghadhabu yake. Amenifukuzia mbali na kunifanya nitembee gizani wala si katika nuru; hakika, amegeuza mkono wake dhidi yangu tena na tena, mchana kutwa. Amefanya ngozi yangu na nyama yangu kuchakaa na ameivunja mifupa yangu. Amenizingira na kunizunguka kwa uchungu na taabu. Amenifanya niishi gizani kama wale waliokufa. Amenizungushia ukuta ili nisiweze kutoroka, amenifunga kwa minyororo mizito. Hata ninapoita au kulia ili kuomba msaada, anakataa kupokea maombi yangu. Ameizuia njia yangu kwa mapande ya mawe, amepotosha njia zangu. Kama dubu aviziaye, kama simba mafichoni, ameniburuta kutoka njia, akanirarua na kuniacha bila msaada. Amevuta upinde wake na kunifanya mimi niwe lengo kwa ajili ya mishale yake. Alinichoma moyo wangu kwa mishale iliyotoka kwenye podo lake. Nimekuwa kichekesho kwa watu wangu wote, wananidhihaki kwa wimbo mchana kutwa. Amenijaza kwa majani machungu na kunishibisha kwa nyongo. Amevunja meno yangu kwa changarawe, amenikanyagia mavumbini. Amani yangu imeondolewa, nimesahau kufanikiwa ni nini. Kwa hiyo nasema, “Fahari yangu imeondoka na yale yote niliyokuwa nimetarajia kutoka kwa BWANA.” Nayakumbuka mateso yangu na kutangatanga kwangu, uchungu na nyongo. Ninayakumbuka vyema, nayo nafsi yangu imezimia ndani yangu.