Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maombolezo 3:45-66

Maombolezo 3:45-66 NEN

Umetufanya takataka na uchafu miongoni mwa mataifa. “Adui zetu wote wamefumbua vinywa vyao wazi dhidi yetu. Tumeteseka kwa hofu kuu na shida ya ghafula, uharibifu na maangamizi.” Vijito vya machozi vinatiririka kutoka machoni mwangu, kwa sababu watu wangu wameangamizwa. Macho yangu yatatiririka machozi bila kukoma, bila kupata nafuu, hadi BWANA atazame chini kutoka mbinguni na kuona. Lile ninaloliona huniletea huzuni nafsini kwa sababu ya wanawake wote wa mji wangu. Wale waliokuwa adui zangu bila sababu wameniwinda kama ndege. Walijaribu kukomesha maisha yangu ndani ya shimo na kunitupia mawe; maji yalifunika juu ya kichwa changu, nami nikafikiri nilikuwa karibu kukatiliwa mbali. Nililiitia jina lako, Ee BWANA, kutoka vina vya shimo. Ulisikia ombi langu: “Usikizibie masikio yako kilio changu nikuombapo msaada.” Ulikuja karibu nilipokuita, nawe ukasema, “Usiogope.” Ee Bwana, ulichukua shauri langu, ukaukomboa uhai wangu. Umeona, Ee BWANA, ubaya niliotendewa. Tetea shauri langu! Umeona kina cha kisasi chao, mashauri yao yote mabaya dhidi yangu. Ee BWANA, umesikia matukano yao, mashauri yao yote mabaya dhidi yangu: kile adui zangu wanachonongʼona na kunungʼunikia dhidi yangu mchana kutwa. Watazame! Wakiwa wameketi au wamesimama, wananidhihaki katika nyimbo zao. Uwalipe kile wanachostahili, Ee BWANA, kwa yale ambayo mikono yao imetenda. Weka pazia juu ya mioyo yao, laana yako na iwe juu yao! Wafuatilie katika hasira na uwaangamize kutoka chini ya mbingu za BWANA.