Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Walawi Utangulizi

Utangulizi
Kitabu cha Walawi kinajulikana kama “Kitabu cha Makuhani,” jina lililotokana na tafsiri ya Maandiko Matakatifu kwa Kiyunani. Walawi walichaguliwa na Mwenyezi Mungu kuwa makuhani. Kitabu cha Walawi kina amri nyingi walizopaswa kuzitii na kuzitenda. Kazi ya ukuhani ilikuwa ya kushughulikia matatizo ya kila siku kuhusu uadilifu wa Waisraeli wote, jinsi ya kumwabudu Mwenyezi Mungu, na kuishi katika utakatifu kama watu wateule wa Mwenyezi Mungu.
Katika Maandiko Matakatifu, Mwenyezi Mungu aliamuru kutolewa kwa sadaka na dhabihu, nazo zikapata maana kutokana na uhusiano wa agano la Mwenyezi Mungu na Israeli. Makusanyiko matakatifu yaliyofanyika katika mwaka yalitoa mwito kwa Waisraeli kufanya upya tabia na ile hali ya kutambua wajibu wao kama watu waliochaguliwa na Mwenyezi Mungu. Ondoleo la dhambi lilifanyika kupitia kumwaga damu wakati wanyama walipokuwa wanatolewa dhabihu, kufuatana na maelekezo yaliyokuwa yametolewa kupitia kwa Musa.
Mwandishi
Musa.
Kusudi
Kuonesha kwa undani sheria zilizowaongoza Waisraeli, yaani makuhani pamoja na watu, katika agano la uhusiano na Mwenyezi Mungu.
Mahali
Chini ya Mlima Sinai, wakati wa safari ya Waisraeli.
Tarehe
Mnamo 1450–1410 K.K.
Wahusika Wakuu
Walawi, Musa, Haruni (na wanawe Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari), na Walawi wote.
Wazo Kuu
Kitabu hiki cha tatu miongoni mwa Vitabu Vitano vya Musa, kimsingi kinashughulikia jinsi ya kuishi maisha matakatifu na kumwabudu Mwenyezi Mungu.
Mambo Muhimu
Utakatifu umetajwa mara nyingi katika kitabu hiki kuliko kitabu kingine chochote cha Maandiko Matakatifu. Mwenyezi Mungu anawafundisha Waisraeli jinsi ya kuishi maisha matakatifu: Mwenyezi Mungu mtakatifu, ukuhani mtakatifu, watu watakatifu, dhabihu takatifu, vyombo vitakatifu, vyakula vitakatifu, pamoja na sheria ya utakatifu kwa ajili ya maisha ya utaua.
Yaliyomo
Amri na maelekezo ya kutoa dhabihu na sadaka (1:1–7:38)
Haruni na wanawe wateuliwa na Mwenyezi Mungu kuwa makuhani (8:1–10:20)
Sheria zinazosimamia usafi na unajisi (11:1–15:33)
Siku ya Upatanisho (16:1-34)
Sheria za utakatifu kimatendo (17:1–22:33)
Sikukuu zilizoamriwa, na mambo mengine (23:1–24:23)
Miaka maalum (25:1-55)
Mambo ya kufanya ili kustahili baraka za Mwenyezi Mungu (26:1–27:34).

Iliyochaguliwa sasa

Walawi Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia