Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka Utangulizi

Utangulizi
Luka alikuwa tabibu. Utangulizi wa Injili ya Luka na ule wa Matendo ya Mitume zinaunganisha vitabu hivi pamoja. Vyote viliandikiwa mtu maarufu wa Kiyunani aliyeitwa Theofilo (maana yake ni Mpendwa wa Mwenyezi Mungu). Lugha na mtindo wa Injili ya Luka na pia Matendo unaonesha kuwa alikuwa mtaalamu mwenye uwezo mkubwa wa kuandika kwa ufasaha, aliyekuwa na elimu ya juu, na asili na mtazamo wa Kiyunani.
Inaaminika kwamba Luka alikuwa mtu wa Mataifa aliyeokoka kutoka Antiokia ya Siria. Aliungana na Paulo huko Troa katika safari ya Paulo ya pili kueneza Injili. Ingawa kuna kazi nyingine nyingi kumhusu Al-Masihi, Luka alitoa mpangilio na mtiririko wa matukio kama mwana-historia ambaye alikuwa na habari za kina, na mwenye uwezo wa kuandika na kutoa habari za kuaminika.
Mwandishi
Luka.
Kusudi
Kudhihirisha habari sahihi za maisha ya Al-Masihi, na kuthibitisha kwamba Al-Masihi ni Mwenyezi Mungu na pia Mwanadamu mkamilifu aliyekuja duniani kwa huduma ya ukombozi wa mwanadamu.
Mahali
Rumi au Kaisaria.
Tarehe
Mnamo 60 B.K.
Wahusika Wakuu
Isa na wanafunzi wake, Elizabeti na Zakaria, Yahya na wanafunzi wake, Mariamu, Herode Mkuu, Pilato, na Mariamu Magdalene.
Wazo Kuu
Luka anaeleza asili ya Umasiya wa Isa, na kusudi la huduma yake.
Mambo Muhimu
Luka anadhihirisha kazi na mafundisho ya Isa, hasa kuelewa mpango wa wokovu, maombi ya Isa, uhusiano wake na watu maskini na watu wa Mataifa waliotengwa na Wayahudi, na kudhihirisha kuhusu Roho wa Mungu. Injili ya Luka ndiyo ndefu kuliko zote.
Yaliyomo
Utangulizi; kuzaliwa kwa Isa na ujana wake (1:1–2:52)
Yahya na Isa, na kujaribiwa kwa Isa (3:1–4:13)
Huduma ya Isa huko Galilaya (4:14–9:50)
Safari ya Isa kwenda Yerusalemu (9:51–19:44)
Huduma ya Isa huko Yerusalemu (19:45–20:47)
Unabii kuhusu mambo yajayo (21:1-38)
Kufa na kufufuka kwa Isa (22:1–24:53).

Iliyochaguliwa sasa

Luka Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia