Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Marko 10:1-12

Marko 10:1-12 NEN

Yesu akaondoka huko, akavuka Mto Yordani, akaenda sehemu za Uyahudi. Umati mkubwa wa watu ukaenda kwake tena, naye kama ilivyokuwa desturi yake, akawafundisha. Baadhi ya Mafarisayo wakaja ili kumjaribu kwa kumuuliza, “Je, ni halali mtu kumwacha mke wake?” Yesu akawajibu, “Je, Mose aliwaamuru nini?” Wakajibu, “Mose aliruhusu kwamba mume anaweza kumwandikia mkewe hati ya talaka na kumwacha.” Yesu akawaambia, “Mose aliwaandikia sheria hiyo kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. Lakini tangu mwanzo wa uumbaji, ‘Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke. Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja.’ Kwa hiyo hawatakuwa wawili tena, bali mwili mmoja. Basi, alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.” Walipokuwa tena ndani ya nyumba, wanafunzi wake wakamuuliza kuhusu jambo hili. Akawajibu, “Mtu yeyote amwachaye mkewe na kuoa mke mwingine, anazini naye. Naye mwanamke amwachaye mumewe na kuolewa na mume mwingine, anazini.”

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Marko 10:1-12