Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Marko 10:1-12

Marko 10:1-12 BHN

Yesu alitoka hapo akaenda mkoani Yudea, hata ngambo ya mto Yordani. Umati wa watu ukamwendea tena, naye akawafundisha tena kama ilivyokuwa desturi yake. Basi, Mafarisayo wakamwendea, na kwa kumjaribu wakamwuliza, “Je, ni halali mume kumpa mkewe talaka?” Yesu akawajibu, “Mose aliwapa maagizo gani?” Nao wakasema, “Mose aliagiza mume kumpatia mkewe hati ya talaka na kumwacha.” Yesu akawaambia, “Mose aliwaandikia amri hiyo kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. Lakini tangu kuumbwa ulimwengu, Mungu aliumba mwanamume na mwanamke. Hivyo mwanamume atawaacha baba yake na mama yake, ataungana na mke wake, nao wawili watakuwa mwili mmoja. Kwa hiyo, wao si wawili tena bali mwili mmoja. Basi, alichounganisha Mungu, binadamu asitenganishe.” Walipoingia tena ndani ya nyumba, wanafunzi wake walimwuliza juu ya jambo hilo. Naye akawaambia, “Anayemwacha mkewe na kuoa mwingine, anazini dhidi ya mkewe. Na mwanamke anayemwacha mumewe na kuolewa na mwingine anazini.”

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Marko 10:1-12