Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 18

18
1Mtu ajitengaye na wengine
hufuata matakwa yake mwenyewe;
hupiga vita kila shauri jema.
2Mpumbavu hafurahii ufahamu,
bali hufurahia kutangaza
maoni yake mwenyewe.
3Uovu unapokuja, dharau huja pia;
pamoja na aibu huja lawama.
4Maneno ya kinywa cha mwanadamu ni kina cha maji,
bali chemchemi ya hekima ni kijito kinachobubujika.
5Sio vizuri kumpendelea mtu mwovu,
au kumnyima haki asiye na hatia.
6Midomo ya mpumbavu humletea ugomvi
na kinywa chake hualika kipigo.
7Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake
na midomo yake ni mtego kwa nafsi yake.
8Maneno ya mchongezi ni kama chakula kitamu;
huingia sehemu za ndani sana za mtu.
9Mtu aliye mlegevu katika kazi yake
ni ndugu na yule anayeharibu.
10Jina la Mwenyezi Mungu ni ngome imara,
wenye haki huikimbilia na kuwa salama.
11Mali ya tajiri ni mji wake wenye ngome,
wanaudhania kuwa ukuta usioweza kurukwa.
12Kabla ya anguko moyo wa mtu hujaa kiburi,
bali unyenyekevu hutangulia heshima.
13Yeye ajibuye kabla ya kusikiliza,
huo ni upumbavu wake na aibu yake.
14Roho ya mtu itastahimili katika ugonjwa
bali roho iliyovunjika ni nani awezaye kuistahimili?
15Moyo wa mwenye ufahamu hujipatia maarifa,
masikio ya mwenye hekima huyatafuta maarifa.
16Zawadi humfungulia njia mtoaji,
nayo humleta mbele ya wakuu.
17Yeye aliye wa kwanza kuleta mashtaka huonekana sahihi,
hadi mwingine ajitokezapo na kumuuliza maswali.
18Kupiga kura hukomesha mashindano
na kutenganisha wapinzani wakuu wanaopingana.
19Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kuridhika
kuliko mji uliozungushiwa ngome,
nayo mabishano ni kama malango
ya ngome yenye makomeo.
20Tumbo la mtu litajaa kutokana na tunda la kinywa chake,
atashibishwa mavuno yanayotokana na midomo yake.
21Mauti na uzima viko katika uwezo wa ulimi,
nao wanaoupenda watakula matunda yake.
22Mtu anayepata mke anapata kitu chema,
naye anajipatia kibali kwa Mwenyezi Mungu.
23Mtu maskini huomba kuhurumiwa
bali tajiri hujibu kwa ukali.
24Mtu aliye na rafiki wasioaminika huangamia upesi,
bali yuko rafiki anayeambatana na mtu kwa karibu kuliko ndugu.

Iliyochaguliwa sasa

Mithali 18: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia