Zaburi 11
11
Zaburi 11
Kumtumaini Mwenyezi Mungu
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1Kwa Mwenyezi Mungu ninakimbilia.
Unawezaje basi kuniambia:
“Ruka kama ndege utorokee kwenye mlima wako.
2Hebu tazama, waovu wanapinda nyuta zao;
wanaweka mishale kwenye nyuzi zake
ili wakiwa gizani, wawapige
walio wanyofu wa moyo.
3Wakati misingi imeharibiwa,
mwenye haki anaweza kufanya nini?”
4Mwenyezi Mungu yuko ndani ya Hekalu lake takatifu;
Mwenyezi Mungu yuko kwenye kiti chake cha enzi mbinguni.
Huwaangalia wana wa watu,
macho yake yanawachunguza.
5Mwenyezi Mungu huwachunguza wenye haki,
lakini nafsi yake inachukia waovu
na wale wanaopenda mapigano.
6Atawanyeshea waovu makaa ya moto mkali
na kiberiti kinachowaka;
upepo wenye joto kali ndio fungu lao.
7Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye haki,
yeye hupenda haki.
Wanyofu watauona uso wake.
Iliyochaguliwa sasa
Zaburi 11: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
![None](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2F58%2Fhttps%3A%2F%2Fweb-assets.youversion.com%2Fapp-icons%2Fsw.png&w=128&q=75)
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.