Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 10

10
Zaburi 10#10 Zaburi hii ikiunganishwa na ya 9 zimetungwa kila beti likianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.
Sala kwa ajili ya haki
1Kwa nini, Ee Mwenyezi Mungu, unasimama mbali?
Kwa nini unajificha wakati wa shida?
2Katika kiburi chake, mwovu humtesa maskini,
waovu na wanaswe katika hila wanazozitunga.
3Hujivunia tamaa za moyo wake;
humbariki mlafi na kumtukana Mwenyezi Mungu.
4Katika kiburi chake, mwovu hamtafuti Mungu,
katika mawazo yake yote
hakuna nafasi ya Mungu.
5Njia zake daima hufanikiwa;
hujivuna na amri zako ziko mbali naye,
huwacheka kwa dharau adui zake wote.
6Anajisemea mwenyewe, “Hakuna kitakachonitikisa,
daima nitakuwa na furaha,
kamwe sitakuwa na shida.”
7Kinywa chake kimejaa laana, uongo na vitisho;
shida na ubaya viko chini ya ulimi wake.
8Huvizia karibu na vijiji;
kutoka mafichoni huwanasa wasio na hatia,
akivizia wapitaji.
9Huvizia kama simba aliye mawindoni;
huvizia kumkamata mnyonge,
huwakamata wanyonge na kuwaburuza
katika wavu wake.
10Mateka wake hupondwa, huzimia;
wanaanguka katika nguvu zake.
11Anajisemea mwenyewe, “Mungu amesahau,
huficha uso wake na haoni kabisa.”
12Inuka Mwenyezi Mungu! Inua mkono wako, Ee Mungu.
Usiwasahau wanyonge.
13Kwa nini mtu mwovu anamtukana Mungu?
Kwa nini anajiambia mwenyewe,
“Hataniita nitoe hesabu”?
14Lakini wewe, Ee Mungu, unaona shida na huzuni,
umekubali kuyapokea mkononi mwako.
Mhanga anajisalimisha kwako,
wewe ni msaada wa yatima.
15Vunja mkono wa mtu mbaya na mwovu;
mwite mtu mbaya atoe hesabu ya uovu wake
ambao usingejulikana vinginevyo.
16Mwenyezi Mungu ni Mfalme milele na milele,
mataifa wataangamia watoke nchini mwake.
17Unasikia, Ee Mwenyezi Mungu, shauku ya wanaoonewa;
wewe huwatia moyo, na kusikiliza kilio chao,
18ukiwatetea yatima na waliodhulumiwa,
ili mwanadamu ambaye ni udongo asiogopeshe tena.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 10: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia