Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 9

9
Zaburi 9#9 Zaburi hii ikiunganishwa na ya 10 zimetungwa kila beti likianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.
Shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya haki yake
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa muth-labeni.#9:0 Muth-labeni ni mtajo mmojawapo katika lugha za muziki. Zaburi ya Daudi.
1Ee Mwenyezi Mungu, nitakutukuza kwa moyo wangu wote,
nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu.
2Nitafurahi na kushangilia ndani yako.
Nitaliimbia sifa jina lako, Ewe Uliye Juu Sana.
3Adui zangu wamerudi nyuma,
wamejikwaa na kuangamia mbele zako.
4Kwa maana umetetea haki yangu na msimamo wangu;
umeketi kwenye kiti chako cha enzi,
ukihukumu kwa haki.
5Umekemea mataifa na kuwaangamiza waovu;
umeyafuta majina yao milele na milele.
6Uharibifu usiokoma umempata adui,
umeing’oa miji yao;
hata kumbukumbu lao limetoweka.
7Mwenyezi Mungu anatawala milele,
ameweka kiti chake cha enzi apate kuhukumu.
8Mungu atahukumu ulimwengu kwa haki,
atatawala mataifa kwa haki.
9Mwenyezi Mungu ni kimbilio la wanaodhulumiwa,
ni ngome imara wakati wa shida.
10Wote wanaolijua jina lako watakutumaini wewe,
kwa maana wewe Mwenyezi Mungu,
hujawaacha kamwe wanaokutafuta.
11Mwimbieni Mwenyezi Mungu sifa, amefanywa mtawala Sayuni,
tangazeni miongoni mwa mataifa, yale aliyoyatenda.
12Kwa maana yeye anayelipiza kisasi cha damu hukumbuka,
hapuuzi kilio cha wanaoonewa.
13Ee Mwenyezi Mungu, tazama jinsi walivyo wengi
adui zangu wanaonitesa!
Nihurumie, uniinue kutoka malango ya mauti,
14ili niweze kutangaza sifa zako
katika malango ya Binti Sayuni,
na huko niushangilie wokovu wako.
15Mataifa wameanguka kwenye shimo walilolichimba,
miguu yao imenaswa kwenye wavu waliouficha.
16Mwenyezi Mungu anajulikana kwa haki yake,
waovu wamenaswa katika kazi za mikono yao.
17Waovu wataishia Kuzimu#9:17 Kuzimu kwa Kiebrania ni Sheol, yaani Shimo lisilo na mwisho.,
naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.
18Lakini mhitaji hatasahaulika siku zote,
wala matumaini ya walioonewa hayatapotea.
19Ee Mwenyezi Mungu, inuka, usimwache binadamu ashinde.
Mataifa na yahukumiwe mbele zako.
20Ee Mwenyezi Mungu, wapige kwa hofu,
mataifa na yajue kuwa wao ni watu tu.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 9: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia