Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 119:56-62

Zaburi 119:56-62 NENO

Hili limekuwa zoezi langu: nami ninayatii mausia yako. Ee Mwenyezi Mungu, wewe ni fungu langu, nimeahidi kuyatii maneno yako. Nimetafuta uso wako kwa moyo wangu wote, nihurumie sawasawa na ahadi yako. Nimezifikiri njia zangu na nimeelekeza hatua zangu katika mausia yako. Nitafanya haraka bila kuchelewa kuzitii amri zako. Hata waovu wanifunge kwa kamba, sitasahau sheria yako. Usiku wa manane ninaamka kukushukuru kwa sababu ya sheria zako za haki.