Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 13

13
Zaburi 13
Sala ya kuomba msaada
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1Hadi lini, Ee Mwenyezi Mungu? Je, utanisahau milele?
Utanificha uso wako hadi lini?
2Nitapambana na mawazo yangu hadi lini,
na kila siku kuwa na majonzi moyoni mwangu?
Adui zangu watanishinda hadi lini?
3Nitazame, unijibu, Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu.
Yatie nuru macho yangu,
ama sivyo nitalala usingizi wa mauti.
4Adui yangu atasema, “Nimemshinda,”
nao adui zangu watashangilia nitakapoanguka.
5Lakini ninategemea upendo wako usiokoma;
moyo wangu unashangilia katika wokovu wako.
6Nitamwimbia Mwenyezi Mungu,
kwa kuwa amekuwa mwema kwangu.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 13: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia