Zaburi 136
136
Zaburi 136
Wimbo wa kumshukuru Mwenyezi Mungu
1Mshukuruni Mwenyezi Mungu, kwa kuwa ni mwema.
Fadhili zake zadumu milele.
2Mshukuruni Mungu wa miungu.
Fadhili zake zadumu milele.
3Mshukuruni Bwana wa mabwana:
Fadhili zake zadumu milele.
4Kwake yeye pekee atendaye maajabu makuu,
Fadhili zake zadumu milele.
5Ambaye kwa ufahamu wake aliziumba mbingu,
Fadhili zake zadumu milele.
6Ambaye aliitandaza dunia juu ya maji,
Fadhili zake zadumu milele.
7Ambaye aliumba mianga mikubwa,
Fadhili zake zadumu milele.
8Jua litawale mchana,
Fadhili zake zadumu milele.
9Mwezi na nyota vitawale usiku,
Fadhili zake zadumu milele.
10Kwake yeye aliyemuua mzaliwa wa kwanza wa Misri,
Fadhili zake zadumu milele.
11Na kuwatoa Israeli katikati yao,
Fadhili zake zadumu milele.
12Kwa mkono wenye nguvu ulionyooshwa,
Fadhili zake zadumu milele.
13Kwake yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu,
Fadhili zake zadumu milele.
14Na kuwapitisha Israeli katikati yake,
Fadhili zake zadumu milele.
15Lakini alimfagia Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu,
Fadhili zake zadumu milele.
16Kwake yeye aliyewaongoza watu wake katika jangwa,
Fadhili zake zadumu milele.
17Ambaye aliwapiga wafalme wenye nguvu,
Fadhili zake zadumu milele.
18Naye aliwaua wafalme wenye nguvu,
Fadhili zake zadumu milele.
19Sihoni mfalme wa Waamori,
Fadhili zake zadumu milele.
20Ogu mfalme wa Bashani,
Fadhili zake zadumu milele.
21Akatoa nchi yao kuwa urithi,
Fadhili zake zadumu milele.
22Urithi kwa Israeli mtumishi wake,
Fadhili zake zadumu milele.
23Aliyetukumbuka katika unyonge wetu,
Fadhili zake zadumu milele.
24Alituweka huru toka adui zetu,
Fadhili zake zadumu milele.
25Ambaye humpa chakula kila kiumbe.
Fadhili zake zadumu milele.
26Mshukuruni Mungu wa mbinguni,
Fadhili zake zadumu milele.
Iliyochaguliwa sasa
Zaburi 136: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
![None](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2F58%2Fhttps%3A%2F%2Fweb-assets.youversion.com%2Fapp-icons%2Fsw.png&w=128&q=75)
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.