Zaburi 135
135
Zaburi 135
Wimbo wa sifa kwa Mwenyezi Mungu
1Msifuni Mwenyezi Mungu.#135:1 kwa Kiebrania ni Hallelu Yah pia 135:3, 21.
Lisifuni jina la Mwenyezi Mungu,
msifuni, enyi watumishi wa Mwenyezi Mungu,
2ninyi ambao mnatumika ndani ya nyumba ya Mwenyezi Mungu,
katika nyua za nyumba ya Mungu wetu.
3Msifuni Mwenyezi Mungu, kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mwema,
liimbieni sifa jina lake, kwa maana hilo lapendeza.
4Kwa maana Mwenyezi Mungu amemchagua Yakobo kuwa wake mwenyewe,
Israeli kuwa hazina yake ya pekee.
5Ninajua ya kuwa Mwenyezi Mungu ni mkuu,
kwamba Bwana wetu ni mkuu kuliko miungu yote.
6Mwenyezi Mungu hufanya lolote apendalo,
mbinguni na duniani,
katika bahari na vilindi vyake vyote.
7Hufanya mawingu kupanda kutoka miisho ya dunia;
hupeleka miali ya radi pamoja na mvua
na huleta upepo kutoka ghala zake.
8Alimuua mzaliwa wa kwanza wa Misri,
mzaliwa wa kwanza wa wanadamu na wanyama.
9Alipeleka ishara zake na maajabu katikati yako, ee Misri,
dhidi ya Farao na watumishi wake wote.
10Aliyapiga mataifa mengi,
na akaua wafalme wenye nguvu:
11Mfalme Sihoni na Waamori,
Ogu mfalme wa Bashani
na wafalme wote wa Kanaani:
12akatoa nchi yao kuwa urithi,
urithi kwa watu wake Israeli.
13Ee Mwenyezi Mungu, jina lako ladumu milele,
kumbukumbu za fahari zako,
Ee Mwenyezi Mungu, kwa vizazi vyote.
14Maana Mwenyezi Mungu atawathibitisha watu wake,
na kuwahurumia watumishi wake.
15Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu,
zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.
16Zina vinywa, lakini haziwezi kusema,
zina macho, lakini haziwezi kuona;
17zina masikio, lakini haziwezi kusikia,
wala hakuna pumzi katika vinywa vyao.
18Wale wanaozitengeneza watafanana nazo,
vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia.
19Ee nyumba ya Israeli, msifuni Mwenyezi Mungu;
ee nyumba ya Haruni, msifuni Mwenyezi Mungu;
20ee nyumba ya Lawi, msifuni Mwenyezi Mungu;
ninyi mnaomcha, msifuni Mwenyezi Mungu.
21Msifuni Mwenyezi Mungu kutoka Sayuni,
msifuni yeye aishiye Yerusalemu.
Msifuni Mwenyezi Mungu.
Iliyochaguliwa sasa
Zaburi 135: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
![None](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2F58%2Fhttps%3A%2F%2Fweb-assets.youversion.com%2Fapp-icons%2Fsw.png&w=128&q=75)
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.