Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 137:1-9

Zaburi 137:1-9 NENO

Kando ya mito ya Babeli tuliketi, tukaomboleza tulipokumbuka Sayuni. Kwenye miti ya huko tulitundika vinubi vyetu, kwa maana huko hao waliotuteka walitaka tuwaimbie nyimbo; watesi wetu walidai nyimbo za furaha; walisema, “Tuimbieni wimbo mmoja kati ya nyimbo za Sayuni!” Tutaimbaje nyimbo za Mwenyezi Mungu, tukiwa nchi ya kigeni? Nikikusahau wewe, ee Yerusalemu, basi mkono wangu wa kuume na usahau ujuzi wake. Ulimi wangu ushikamane na kaakaa la kinywa changu kama sitakukumbuka wewe, kama nisipokufikiri Yerusalemu kuwa furaha yangu kubwa. Kumbuka, Ee Mwenyezi Mungu, walichokifanya Waedomu, siku ile Yerusalemu ilipoanguka. Walisema, “Bomoa, bomoa hata misingi yake!” Ee binti Babeli, uliyehukumiwa kuangamizwa, heri yeye atakayekulipiza wewe kwa yale uliyotutenda sisi: yeye ambaye atawakamata watoto wako wachanga na kuwaponda juu ya miamba.