Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 137:1-9

Zaburi 137:1-9 SRUV

Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi, Tukalia tulipoikumbuka Sayuni. Katika miti iliyo katikati yake Tulivitundika vinubi vyetu. Maana huko waliotuchukua mateka Walitaka tuwaimbie; Na waliotuonea walitaka tuwatumbuize; Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni. Twawezaje kuimba wimbo wa BWANA Katika nchi ya ugeni? Nikikusahau, Ee Yerusalemu, Mkono wangu wa kulia na upooze. Ulimi wangu na ugandamane Na kaakaa la kinywa changu, nisipokukumbuka. Nisipoikuza Yerusalemu Zaidi ya furaha yangu iliyo kuu. Ee BWANA, uwakumbuke wana wa Edomu, Siku ile Yerusalemu ilipotekwa. Kwa namna walivyosema, Bomoeni! Bomoeni hata misingini! Ee binti Babeli, uliye karibu na kuangamia, Heri atakayekupatiliza, ulivyotupatiliza sisi. Heri yeye atakayewakamata wadogo wako, Na kuwaseta wao juu ya mwamba.

Soma Zaburi 137