Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 137:1-9

Zab 137:1-9 SUV

Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi, Tukalia tulipoikumbuka Sayuni. Katika miti iliyo katikati yake Tulivitundika vinubi vyetu. Maana huko waliotuchukua mateka Walitaka tuwaimbie; Na waliotuonea walitaka furaha; Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni. Tuuimbeje wimbo wa BWANA Katika nchi ya ugeni? Ee Yerusalemu, nikikusahau wewe, Mkono wangu wa kuume na usahau. Ulimi wangu na ugandamane Na kaakaa la kinywa changu, nisipokukumbuka. Nisipoikuza Yerusalemu Zaidi ya furaha yangu iliyo kuu. Ee BWANA, uwakumbuke wana wa Edomu, Siku ya Yerusalemu. Waliosema, Bomoeni! Bomoeni hata misingini! Ee binti Babeli, uliye karibu na kuangamia, Heri atakayekupatiliza, ulivyotupatiliza sisi. Heri yeye atakayewakamata wadogo wako, Na kuwaseta wao juu ya mwamba.