Zaburi 146
146
Zaburi 146
Kumsifu Mwenyezi Mungu mwokozi
1Msifuni Mwenyezi Mungu!#146:1 kwa Kiebrania ni Hallelu Yah; pia 146:10.
Ee nafsi yangu, umsifu Mwenyezi Mungu,
2Nitamsifu Mwenyezi Mungu maisha yangu yote;
nitamwimbia Mungu wangu sifa
wakati wote ningali hai.
3Usiweke tumaini lako kwa wakuu,
kwa wanadamu ambao hufa,
ambao hawawezi kuokoa.
4Roho yao itokapo hurudi mavumbini,
siku hiyo hiyo mipango yao yote hukoma.
5Heri yeye ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake,
ambaye tumaini lake ni katika Mwenyezi Mungu, Mungu wake,
6Muumba wa mbingu na nchi,
na bahari na vyote vilivyomo:
Mwenyezi Mungu anayedumu kuwa mwaminifu
milele na milele.
7Naye huwapatia haki waliodhulumiwa,
na kuwapa wenye njaa chakula.
Mwenyezi Mungu huwaweka wafungwa huru,
8Mwenyezi Mungu huwafumbua vipofu macho,
Mwenyezi Mungu huwainua waliolemewa na mizigo yao,
Mwenyezi Mungu huwapenda wenye haki.
9Mwenyezi Mungu huwalinda wageni
na kuwategemeza yatima na wajane,
lakini hupinga njia za waovu.
10Mwenyezi Mungu atamiliki milele,
Mungu wako, ee Sayuni,
kwa vizazi vyote.
Msifuni Mwenyezi Mungu.
Iliyochaguliwa sasa
Zaburi 146: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.