Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 148

148
Zaburi 148
Mwito kwa ulimwengu kumsifu Mwenyezi Mungu
1Msifuni Mwenyezi Mungu.#148:1 kwa Kiebrania ni Hallelu Yah; pia 148:7, 14.
Msifuni Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni,
msifuni juu vileleni.
2Msifuni, enyi malaika wake wote,
msifuni yeye, enyi jeshi lake lote la mbinguni.
3Msifuni yeye, enyi jua na mwezi,
msifuni yeye, enyi nyota zote zinazong’aa.
4Msifuni yeye, enyi mbingu zilizo juu sana,
na ninyi maji juu ya anga.
5Vilisifu jina la Mwenyezi Mungu
kwa maana aliamuru navyo vikaumbwa.
6Aliviweka mahali pake milele na milele,
alitoa amri ambayo haibadiliki milele.
7Msifuni Mwenyezi Mungu kutoka duniani,
ninyi wanyama wakubwa wa baharini,
na vilindi vyote vya bahari,
8miali ya radi na mvua ya mawe, theluji na mawingu,
pepo za dhoruba zinazotimiza amri zake,
9ninyi milima na vilima vyote,
miti ya matunda na mierezi yote,
10wanyama pori na mifugo yote,
viumbe vidogo na ndege warukao,
11wafalme wa dunia na mataifa yote,
ninyi wakuu na watawala wote wa dunia,
12vijana wa kiume na wanawali,
wazee na watoto.
13Wote na walisifu jina la Mwenyezi Mungu,
kwa maana jina lake pekee limetukuka,
utukufu wake uko juu ya nchi na mbingu.
14Amewainulia watu wake pembe#148:14 pembe inawakilisha mwenye nguvu, yaani mfalme,
sifa ya watakatifu wake wote,
ya Israeli, watu walio karibu na moyo wake.
Msifuni Mwenyezi Mungu.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 148: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia