Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 149

149
Zaburi 149
Wimbo wa kumsifu Mwenyezi Mungu kwa wema wake
1Msifuni Mwenyezi Mungu.#149:1 kwa Kiebrania ni Hallelu Yah; pia 149:9.
Mwimbieni Mwenyezi Mungu wimbo mpya,
sifa zake katika kusanyiko la watakatifu.
2Israeli na washangilie katika Muumba wao,
watu wa Sayuni na wafurahi katika Mfalme wao.
3Na walisifu jina lake kwa kucheza
na wampigie muziki kwa matari na kinubi.
4Kwa maana Mwenyezi Mungu anapendezwa na watu wake,
anawavika wanyenyekevu taji la wokovu.
5Watakatifu washangilie katika heshima hii,
na waimbe kwa shangwe vitandani mwao.
6Sifa za Mungu na ziwe vinywani mwao
na upanga ukatao kuwili mikononi mwao,
7ili walipize mataifa kisasi
na adhabu juu ya mataifa,
8wawafunge wafalme wao kwa minyororo,
wakuu wao kwa pingu za chuma,
9ili kuwafanyia hukumu iliyoandikwa dhidi yao.
Huu ndio utukufu wa watakatifu wake wote.
Msifuni Mwenyezi Mungu.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 149: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia