Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 46:1-7

Zaburi 46:1-7 NENO

Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa, hata kama dunia ikiondolewa, na milima ianguke kilindini cha bahari, hata maji yake yakinguruma na kuumuka, na milima itetemeke kwa mawimbi yake. Kuna mto ambao vijito vyake vinaufurahisha mji wa Mungu, mahali patakatifu ambako Aliye Juu Sana anaishi. Mungu yuko katikati yake, hautaanguka, Mungu atausaidia asubuhi na mapema. Mataifa yanafanya ghasia, falme zinaanguka, yeye hupaza sauti yake, dunia ikayeyuka. Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni yu pamoja nasi; Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.