Zaburi 78:32-39
Zaburi 78:32-39 NENO
Licha ya haya yote, waliendelea kutenda dhambi, licha ya maajabu yake, hawakuamini. Kwa hiyo akamaliza siku zao katika ubatili na miaka yao katika vitisho. Kila mara Mungu alipowaua baadhi yao, waliosalia walimtafuta, walimgeukia tena kwa shauku. Walikumbuka kwamba Mungu alikuwa Mwamba wao, kwamba Mungu Aliye Juu Sana alikuwa Mkombozi wao. Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao, wakisema uongo kwa ndimi zao, mioyo yao haikuwa thabiti kwake, wala hawakuwa waaminifu katika agano lake. Hata hivyo alikuwa na huruma, alisamehe maovu yao na hakuwaangamiza. Mara kwa mara alizuia hasira yake, wala hakuchochea ghadhabu yake yote. Alikumbuka kwamba wao walikuwa nyama tu, upepo upitao ambao haurudi.