Zaburi 78:32-39
Zaburi 78:32-39 Biblia Habari Njema (BHN)
Hata hivyo waliendelea kumkosea Mungu; ijapokuwa alitenda maajabu, hawakuamini. Basi, akazikatisha siku zao kama pumzi, miaka yao kwa maafa ya ghafla. Kila alipowaua, waliobaki walimgeukia; walitubu, wakamgeukia Mungu kwa moyo. Walikumbuka kwamba Mungu alikuwa mwamba wao; Mungu Mkuu alikuwa mkombozi wao. Lakini walimdanganya kwa maneno yao; kila walichomwambia kilikuwa uongo. Hawakuambatana naye kwa moyo, hawakuwa waaminifu kwa agano lake. Lakini Mungu mwenye huruma alisamehe uovu wao, na wala hakuwaangamiza. Mara nyingi aliizuia hasira yake, wala hakuiacha ghadhabu yake yote iwake. Alikumbuka kwamba wao ni watu tu; ni kama upepo upitao na kutoweka.
Zaburi 78:32-39 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Pamoja na hayo wakazidi kutenda dhambi, Wala hawakuyaamini matendo yake ya ajabu. Kwa hiyo akazikomesha siku zao kama pumzi, Na miaka yao kwa hofu ya kuwastusha. Alipowaua ndipo walipokuwa wakimtafuta; Wakarudi wakamtaka Mungu kwa bidii. Wakakumbuka kuwa Mungu ni mwamba wao, Na Mungu Aliye Juu ni mkombozi wao. Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao, Wakamwambia uongo kwa ndimi zao. Kwa maana mioyo yao haikuwa thabiti kwake, Wala hawakuwa waaminifu katika agano lake. Lakini Yeye, kwa kuwa anayo rehema, Husamehe uovu wala haangamizi. Mara nyingi huipishia mbali ghadhabu yake, Wala haiwashi hasira yake yote. Akakumbuka ya kuwa wao ni kiwiliwili, Upepo upitao wala haurudi.
Zaburi 78:32-39 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Pamoja na hayo wakazidi kutenda dhambi, Wala hawakuyaamini matendo yake ya ajabu. Kwa hiyo akazikomesha siku zao kama pumzi, Na miaka yao kwa hofu ya kuwasitusha. Alipowaua ndipo walipokuwa wakimtafuta; Wakarudi wakamtaka Mungu kwa bidii. Wakakumbuka kuwa Mungu ni mwamba wao, Na Mungu Aliye juu ni mkombozi wao. Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao, Wakamwambia uongo kwa ndimi zao. Kwa maana mioyo yao haikuwa thabiti kwake, Wala hawakuwa waaminifu katika agano lake. Lakini Yeye, kwa kuwa anayo rehema, Husamehe uovu wala haangamizi. Mara nyingi huipishia mbali ghadhabu yake, Wala haiwashi hasira yake yote. Akakumbuka ya kuwa wao ni kiwiliwili, Upepo upitao wala haurudi.
Zaburi 78:32-39 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Licha ya haya yote, waliendelea kutenda dhambi, licha ya maajabu yake, hawakuamini. Kwa hiyo akamaliza siku zao katika ubatili na miaka yao katika vitisho. Kila mara Mungu alipowaua baadhi yao, waliosalia walimtafuta, walimgeukia tena kwa shauku. Walikumbuka kwamba Mungu alikuwa Mwamba wao, kwamba Mungu Aliye Juu Sana alikuwa Mkombozi wao. Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao, wakisema uongo kwa ndimi zao, mioyo yao haikuwa thabiti kwake, wala hawakuwa waaminifu katika agano lake. Hata hivyo alikuwa na huruma, alisamehe maovu yao na hakuwaangamiza. Mara kwa mara alizuia hasira yake, wala hakuchochea ghadhabu yake yote. Alikumbuka kwamba wao walikuwa nyama tu, upepo upitao ambao haurudi.