Ruthu 1:20-21
Ruthu 1:20-21 NENO
Akawaambia, “Msiniite tena Naomi; niiteni Mara, kwa sababu Mwenyezi amenitendea mambo machungu sana. Mimi niliondoka hali nimejaa, lakini Mwenyezi Mungu amenirudisha mtupu. Kwa nini kuniita Naomi? Mwenyezi Mungu amenitendea mambo machungu; Mwenyezi ameniletea msiba.”