Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zekaria 10:1-3

Zekaria 10:1-3 NEN

Mwombeni BWANA mvua wakati wa vuli; ndiye BWANA atengenezaye mawingu ya tufani. Huwapa watu manyunyu ya mvua, pia mimea ya shambani kwa ajili ya kila mtu. Sanamu huzungumza udanganyifu, waaguzi huona maono ya uongo; husimulia ndoto ambazo si za kweli, wanatoa faraja batili. Kwa hiyo watu wanatangatanga kama kondoo walioonewa kwa kukosa mchungaji. “Hasira yangu inawaka dhidi ya wachungaji, nami nitawaadhibu viongozi; kwa kuwa BWANA Mwenye Nguvu Zote atalichunga kundi lake, nyumba ya Yuda, naye atawafanya kuwa kama farasi mwenye kiburi akiwa vitani.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zekaria 10:1-3