Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zekaria 11:1-3

Zekaria 11:1-3 NEN

Fungua milango yako, ee Lebanoni, ili moto uteketeze mierezi yako! Piga yowe, ee mti wa msunobari, kwa kuwa mwerezi umeanguka; miti ya fahari imeharibiwa! Piga yowe, enyi mialoni ya Bashani, msitu mnene umefyekwa! Sikiliza yowe la wachungaji; malisho yao manono yameangamizwa! Sikia ngurumo za simba; kichaka kilichostawi sana cha Yordani kimeharibiwa!