1 Kor 13
13
Karama ya Upendo
1Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. 2#Mt 17:20; 7:22; 21:21; Mk 11:23Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. 3#Mt 6:2Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu. 4Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; 5#Zek 8:17; Flp 2:4haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; 6#Rum 12:9haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; 7#Mit 10:12; 1 Kor 9:12; Rum 15:1huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. 8#1 Pet 4:8Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika. 9Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu; 10lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika. 11Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto. 12#2 Kor 5:7; Yak 1:23Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana. 13#1 The 1:3; 1 Yoh 4:16Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.
Iliyochaguliwa sasa
1 Kor 13: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.