1
1 Kor 13:4-5
Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia
Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya
Linganisha
Chunguza 1 Kor 13:4-5
2
1 Kor 13:7
huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
Chunguza 1 Kor 13:7
3
1 Kor 13:6
haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli
Chunguza 1 Kor 13:6
4
1 Kor 13:13
Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.
Chunguza 1 Kor 13:13
5
1 Kor 13:8
Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
Chunguza 1 Kor 13:8
6
1 Kor 13:1
Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
Chunguza 1 Kor 13:1
7
1 Kor 13:2
Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.
Chunguza 1 Kor 13:2
8
1 Kor 13:3
Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.
Chunguza 1 Kor 13:3
9
1 Kor 13:11
Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto.
Chunguza 1 Kor 13:11
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video