Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayu 30:16-31

Ayu 30:16-31 SUV

Sasa nafsi yangu inamwagika ndani yangu; Siku za mateso zimenishika. Wakati wa usiku mifupa yangu huchomeka ndani yangu, Na maumivu yanayonitafuna hayapumziki. Kwa ugonjwa wangu kuwa na nguvu nyingi Mavazi yangu yameharibika; Hunikaza kama shingo ya kanzu yangu. Yeye amenibwaga topeni, Nami nimekuwa kama mavumbi na majivu. Nakulilia wewe, wala huniitikii; Nasimama, nawe wanitazama tu. Wewe umegeuka kuwa mkali kwangu; Nawe waniudhi kwa uweza wa mkono wako. Waniinua juu hata upeponi, na kunipandisha juu yake; Nawe waniyeyusha katika dhoruba. Kwani najua kuwa utanileta hata kifoni, Niifikilie nyumba waliyoandikiwa wenye uhai wote. Je! Mtu katika kuanguka kwake hanyoshi mkono? Na kulilia msaada katika msiba wake? Je! Mimi sikulia kwa ajili ya huyo aliyekuwa katika taabu? Nafsi yangu, je! Haikusononeka kwa ajili ya wahitaji? Hapo nilipotazamia mema, ndipo yakaja mabaya; Nami nilipongojea mwanga, likaja giza. Matumbo yangu yatokota, wala hayaachi; Siku za taabu zimenijilia. Naenda nikiomboleza pasipo jua; Nasimama katika mkutano, na kuulilia msaada. Mimi ni ndugu yao mbwa-mwitu, Ni mwenzao mbuni. Ngozi yangu ni nyeusi, nayo yanitoka, Na mifupa yangu imeteketea kwa hari. Kwa hiyo kinanda changu kimegeuzwa kuwa maombolezo, Na filimbi yangu kuwa sauti yao waliao.