Yobu 30:16-31
Yobu 30:16-31 Biblia Habari Njema (BHN)
“Sasa sina nguvu yoyote nafsini mwangu; siku za mateso zimenikumba. Usiku mifupa yangu yote huuma, maumivu yanayonitafuna hayapoi. Mungu amenikaba kwa mavazi yangu, amenibana kama ukosi wa shati langu. Amenibwaga matopeni; nimekuwa kama majivu na mavumbi. Nakulilia, lakini hunijibu, nasimama kuomba lakini hunisikilizi. Umegeuka kuwa mkatili kwangu, wanitesa kwa mkono wako wenye nguvu. Wanitupa katika upepo na kunipeperusha; wanisukasuka huku na huko katika dhoruba kali. Naam! Najua utanipeleka tu kifoni, mahali watakapokutana wote waishio. “Je, mtu akikumbwa na maangamizi hainui mkono? Je, mtu akiwa taabuni haombi msaada Je, sikuwalilia wale waliokuwa na taabu? Je, sikuona uchungu kwa ajili ya maskini? Lakini nilipotazamia mema, mabaya yalinipata, nilipongojea mwanga, giza lilikuja. Moyo wangu wahangaika wala hautulii kamwe; siku za mateso zimekumbana nami. Napitapita nikiomboleza, kwangu hamna jua. Nasimama hadharani kuomba msaada. Kwa kilio nimekuwa ndugu yake mbwamwitu, mimi na mbuni hamna tofauti. Ngozi yangu imebambuka mifupa yangu inaungua kwa homa. Kinubi changu kimekuwa cha kufanya matanga filimbi yangu kwa ajili ya kuomboleza.
Yobu 30:16-31 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Sasa nafsi yangu inamwagika ndani yangu; Siku za mateso zimenishika. Wakati wa usiku mifupa yangu huchomeka ndani yangu, Na maumivu yanayonitafuna hayapumziki. Kwa ugonjwa wangu kuwa na nguvu nyingi Mavazi yangu yameharibika; Hunikaza kama shingo ya kanzu yangu. Yeye amenibwaga topeni, Nami nimekuwa kama mavumbi na majivu. Nakulilia wewe, wala huniitikii; Nasimama, nawe wanitazama tu. Wewe umegeuka kuwa mkali kwangu; Nawe waniudhi kwa uweza wa mkono wako. Waniinua juu hata upeponi, na kunipandisha juu yake; Nawe waniyeyusha katika dhoruba. Kwani najua kuwa utanileta hata kifoni, Niifikie nyumba waliyoaandaliwa wenye uhai wote. Je! Mtu katika kuanguka kwake hanyoshi mkono? Na kulilia msaada katika msiba wake? Je! Mimi sikulia kwa ajili ya huyo aliyekuwa katika taabu? Nafsi yangu, je! Haikusononeka kwa ajili ya wahitaji? Hapo nilipotazamia mema, ndipo yakaja mabaya; Nami nilipongojea mwanga, likaja giza. Matumbo yangu yatokota, wala hayaachi; Siku za taabu zimenijia. Naenda nikiomboleza pasipo jua; Nasimama katika mkutano, na kuulilia msaada. Mimi ni ndugu yao mbwamwitu, Ni mwenzao mbuni. Ngozi yangu ni nyeusi, nayo yanitoka, Na mifupa yangu imeteketea kwa joto. Kwa hiyo kinanda changu kimegeuzwa kuwa maombolezo, Na filimbi yangu kuwa sauti yao waliao.
Yobu 30:16-31 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Sasa nafsi yangu inamwagika ndani yangu; Siku za mateso zimenishika. Wakati wa usiku mifupa yangu huchomeka ndani yangu, Na maumivu yanayonitafuna hayapumziki. Kwa ugonjwa wangu kuwa na nguvu nyingi Mavazi yangu yameharibika; Hunikaza kama shingo ya kanzu yangu. Yeye amenibwaga topeni, Nami nimekuwa kama mavumbi na majivu. Nakulilia wewe, wala huniitikii; Nasimama, nawe wanitazama tu. Wewe umegeuka kuwa mkali kwangu; Nawe waniudhi kwa uweza wa mkono wako. Waniinua juu hata upeponi, na kunipandisha juu yake; Nawe waniyeyusha katika dhoruba. Kwani najua kuwa utanileta hata kifoni, Niifikilie nyumba waliyoandikiwa wenye uhai wote. Je! Mtu katika kuanguka kwake hanyoshi mkono? Na kulilia msaada katika msiba wake? Je! Mimi sikulia kwa ajili ya huyo aliyekuwa katika taabu? Nafsi yangu, je! Haikusononeka kwa ajili ya wahitaji? Hapo nilipotazamia mema, ndipo yakaja mabaya; Nami nilipongojea mwanga, likaja giza. Matumbo yangu yatokota, wala hayaachi; Siku za taabu zimenijilia. Naenda nikiomboleza pasipo jua; Nasimama katika mkutano, na kuulilia msaada. Mimi ni ndugu yao mbwa-mwitu, Ni mwenzao mbuni. Ngozi yangu ni nyeusi, nayo yanitoka, Na mifupa yangu imeteketea kwa hari. Kwa hiyo kinanda changu kimegeuzwa kuwa maombolezo, Na filimbi yangu kuwa sauti yao waliao.
Yobu 30:16-31 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
“Sasa maisha yangu yamefikia mwisho; siku za mateso zimenikamata. Usiku mifupa yangu inachoma; maumivu yanayonitafuna hayatulii kamwe. Kwa uwezo wake mkuu Mungu huwa kwangu kama nguo; hushikamana nami kama ukosi wa vazi langu. Yeye amenitupa kwenye matope, nami nimekuwa kama mavumbi na majivu. “Ee Mwenyezi Mungu, ninakulilia wewe lakini hunijibu; ninasimama, nawe unanitazama tu. Wewe unanigeukia bila huruma; unanishambulia kwa nguvu za mkono wako. Unaninyakua na kunipeperusha kwa upepo; umenirusharusha kwenye dhoruba. Ninajua utanileta hadi kifoni, mahali wenye uhai wote wamewekewa. “Hakika hakuna mtu anayemshambulia mhitaji anapoomba msaada katika shida yake. Je, sikulia kwa ajili ya wale waliokuwa katika taabu? Je, nafsi yangu haikusononeka kwa ajili ya maskini? Lakini nilipotazamia mema, mabaya yalinijia; nilipotafuta nuru, ndipo giza lilipokuja. Kusukwasukwa ndani yangu kamwe hakutulii; siku za mateso zinanikabili. Ninazunguka nikiwa nimeungua, lakini si kwa jua; ninasimama katika kusanyiko nikiomba msaada. Nimekuwa ndugu wa mbweha, rafiki wa mabundi. Ngozi yangu imekuwa nyeusi nayo inachunika; mifupa yangu inaungua kwa homa. Kinubi changu kimegeuka kuwa maombolezo, nayo filimbi yangu imekuwa sauti ya kilio.