Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yobu 30:16-31

Yobu 30:16-31 BHN

“Sasa sina nguvu yoyote nafsini mwangu; siku za mateso zimenikumba. Usiku mifupa yangu yote huuma, maumivu yanayonitafuna hayapoi. Mungu amenikaba kwa mavazi yangu, amenibana kama ukosi wa shati langu. Amenibwaga matopeni; nimekuwa kama majivu na mavumbi. Nakulilia, lakini hunijibu, nasimama kuomba lakini hunisikilizi. Umegeuka kuwa mkatili kwangu, wanitesa kwa mkono wako wenye nguvu. Wanitupa katika upepo na kunipeperusha; wanisukasuka huku na huko katika dhoruba kali. Naam! Najua utanipeleka tu kifoni, mahali watakapokutana wote waishio. “Je, mtu akikumbwa na maangamizi hainui mkono? Je, mtu akiwa taabuni haombi msaada Je, sikuwalilia wale waliokuwa na taabu? Je, sikuona uchungu kwa ajili ya maskini? Lakini nilipotazamia mema, mabaya yalinipata, nilipongojea mwanga, giza lilikuja. Moyo wangu wahangaika wala hautulii kamwe; siku za mateso zimekumbana nami. Napitapita nikiomboleza, kwangu hamna jua. Nasimama hadharani kuomba msaada. Kwa kilio nimekuwa ndugu yake mbwamwitu, mimi na mbuni hamna tofauti. Ngozi yangu imebambuka mifupa yangu inaungua kwa homa. Kinubi changu kimekuwa cha kufanya matanga filimbi yangu kwa ajili ya kuomboleza.

Soma Yobu 30