Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayu 39:1-12

Ayu 39:1-12 SUV

Je! Wajua majira ya kuzaa kwao mbuzi-mwitu walio majabalini? Au waweza kusema majira ya kuzaa kulungu? Je! Waweza kuhesabu miezi yao watakayoitimiza? Au je! Wajua majira ya kuzaa kwao? Wao hujiinamisha, kuzaa watoto wao, Watupa taabu zao. Watoto wao wa katika hali nzuri, hukua katika bara wazi; Huenda zao, wala hawarudi tena. Ni nani aliyempeleka punda-milia aende huru? Au je! Ni nani aliyemfungulia vifungo punda-mwitu? Ambaye nimeifanya nyika kuwa nyumba yake, Na nchi ya chumvi kuwa makao yake. Yeye hudharau mshindo wa mji, Wala hasikii kelele zake msimamizi. Upana wa milima ni malisho yake, Hutafuta-tafuta kila kitu kilicho kibichi. Je! Nyati atakubali kukutumikia? Au atakaa katika zizi lako? Je! Waweza kumfunga nyati kwa kamba matutani? Au, yeye atayalima mabonde nyuma yako? Je! Utamtumaini kwa sababu ana nguvu nyingi? Au, utamwachia yeye kazi yako? Je! Utamtumaini kwamba ataileta mbegu yako nyumbani. Na kukusanya nafaka ya kiwanja chako cha kupuria?

Soma Ayu 39