Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayubu 39:1-12

Ayubu 39:1-12 SRUV

Je! Wajua majira ya kuzaa kwao mbuzi-mwitu walio majabalini? Au waweza kusema majira ya kuzaa kwa kulungu? Je! Waweza kuhesabu miezi yao watakayoitimiza? Au waweza kusema majira ya kuzaa kwa kulungu? Wao hujiinamisha, kuzaa watoto wao, Watupa taabu zao. Watoto wao wako katika hali nzuri, hukua katika bara wazi; Huenda zao, wala hawarudi tena. Ni nani aliyemwacha pundamilia aende huru? Au je! Ni nani aliyemfungulia vifungo punda mwitu? Ambaye nimeifanya nyika kuwa nyumba yake, Na nchi ya chumvi kuwa makao yake. Yeye hudharau mshindo wa mji, Wala hasikii kelele zake msimamizi. Upana wa milima ni malisho yake, Hutafutatafuta kila kitu kilicho kibichi. Je! Nyati atakubali kukutumikia? Au atakaa katika zizi lako? Je! Waweza kumfunga nyati kwa kamba matutani? Au, yeye atayalima mabonde nyuma yako? Je! Utamtumaini kwa sababu ana nguvu nyingi? Au, utamwachia yeye kazi yako? Je! Utamtumaini kwamba ataileta mbegu yako nyumbani. Na kukusanya nafaka ya kiwanja chako cha kupuria?

Soma Ayubu 39