Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mt 27

27
Yesu Aletwa mbele ya Pilato
1 # Mk 15:1; Lk 22:66; Yn 18:28 Na ilipokuwa asubuhi, wakuu wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri juu ya Yesu, wapate kumwua; 2#Lk 23:1; Yn 18:31,32wakamfunga, wakamchukua, wakampeleka kwa Pilato aliyekuwa liwali.
Yuda Ajinyonga
3 # Mdo 1:18-19; Mt 26:15 Kisha Yuda, yule mwenye kumsaliti, alipoona ya kuwa amekwisha kuhukumiwa, alijuta, akawarudishia wakuu wa makuhani na wazee vile vipande thelathini vya fedha, akasema, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia. 4Wakasema, Basi, haya yatupasani sisi? Yaangalie haya wewe mwenyewe. 5#Mdo 1:18; 2 Sam 17:23Akavitupa vile vipande vya fedha katika hekalu, akaondoka; akaenda, akajinyonga. 6#Mk 12:41Wakuu wa makuhani wakavitwaa vile vipande vya fedha, wakasema, Si halali kuviweka katika sanduku ya sadaka, kwa kuwa ni kima cha damu. 7Wakafanya shauri, wakavitumia kwa kununua konde la mfinyanzi liwe mahali pa kuzika wageni. 8#Mdo 1:19Kwa hiyo konde lile huitwa konde la damu hata leo. 9#Zek 11:12-13; Yer 32:6-9Ndipo likatimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema, Wakavitwaa vipande thelathini vya fedha, kima chake aliyetiwa kima, ambaye baadhi ya Waisraeli walimtia kima; 10wakavitumia kwa kununua konde la mfinyanzi, kama Bwana alivyoniagiza.
Pilato Amhoji Yesu
11 # Mk 15:2-5; Lk 23:2,3; Yn 18:29-38 Naye Yesu akasimama mbele ya liwali; liwali akamwuliza, akasema, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Yesu akamwambia, Wewe wasema. 12#Mt 26:63; Isa 53:7Lakini aliposhitakiwa na wakuu wa makuhani na wazee, hakujibu hata neno. 13Ndipo Pilato akamwambia, Husikii ni mambo mangapi wanayokushuhudia? 14#Yn 19:9Asimjibu hata neno moja, hata liwali akastaajabu sana. 15#Mk 15:6-15; Lk 23:13-25; Yn 18:39—19:1Basi wakati wa siku kuu, liwali desturi yake huwafungulia mkutano mfungwa mmoja waliyemtaka. 16Basi palikuwa na mfungwa mashuhuri siku zile, aitwaye Baraba. 17Basi walipokutanika, Pilato akawaambia, Mnataka niwafungulie yupi? Yule Baraba, au Yesu aitwaye Kristo? 18#Yn 11:47,48; 12:19Kwa maana alijua ya kuwa wamemtoa kwa husuda.
19Na alipokuwa ameketi juu ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea mjumbe, kumwambia, Usiwe na neno na yule mwenye haki; kwa sababu nimeteswa mengi leo katika ndoto kwa ajili yake.
20Nao wakuu wa makuhani na wazee wakawashawishi makutano ili wamtake Baraba, na kumwangamiza Yesu. 21Basi liwali akajibu, akawaambia, Mnataka niwafungulie yupi katika hawa wawili? Wakasema, Baraba. 22Pilato akawaambia, Basi, nimtendeje Yesu aitwaye Kristo? Wakasema wote, Asulibiwe. 23Akasema, Kwani? Ni ubaya gani alioutenda? Wakazidi sana kupiga kelele, wakisema, Na asulibiwe.
Pilato Amtoa Yesu Asulubiwe
24 # Kum 21:6-9 Basi Pilato alipoona ya kuwa hafai lo lote, bali ghasia inazidi tu, akatwaa maji, akanawa mikono yake mbele ya mkutano, akasema, Mimi sina hatia katika damu ya mtu huyu mwenye haki; yaangalieni haya ninyi wenyewe. 25#Mdo 5:28Watu wote wakajibu wakasema, Damu yake na iwe juu yetu, na juu ya watoto wetu. 26Ndipo akawafungulia Baraba; na baada ya kumpiga Yesu mijeledi, akamtoa ili asulibiwe.
Askari Wamdhihaki Yesu
27 # Mk 15:16-19; Yn 19:2,3 Ndipo askari wa liwali wakamchukua Yesu ndani ya Praitorio,#Praitorio maana yake ni Nyumba ya Uliwali. wakamkusanyikia kikosi kizima. 28Wakamvua nguo, wakamvika vazi jekundu. 29Wakasokota taji ya miiba, wakaiweka juu ya kichwa chake, na mwanzi katika mkono wake wa kuume; wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki, wakisema, Salamu, Mfalme wa Wayahudi! 30#Isa 50:6Kisha wakamtemea mate, wakautwaa ule mwanzi, wakampiga-piga kichwani. 31#Mk 15:20-41; Lk 23:26,33-49; Yn 19:16-30Walipokwisha kumdhihaki, wakalivua lile vazi, wakamvika mavazi yake, wakamchukua kumsulibisha.
Yesu Asulubiwa
32Hata walipokuwa wakitoka, wakamwona mtu Mkirene, jina lake Simoni; huyu wakamshurutisha auchukue msalaba wake. 33Na walipofika mahali paitwapo Golgotha, yaani, Fuvu la kichwa, 34#Zab 69:22wakampa kunywa divai iliyochanganyika na nyongo; lakini yeye alipoionja hakutaka kunywa. 35#Zab 22:19Walipokwisha kumsulibisha, waligawa mavazi yake, wakipiga kura; [ili litimie neno lililonenwa na nabii, Waligawa nguo zangu kati yao, na juu ya vazi langu walipiga kura.] 36Wakaketi, wakamlinda huko. 37Wakaweka juu ya kichwa chake mashitaka yake, yaliyoandikwa HUYU NI YESU, MFALME WA WAYAHUDI. 38#Isa 53:12Wakati uo huo wanyang’anyi wawili wakasulibiwa pamoja naye, mmoja mkono wake wa kuume, na mmoja mkono wake wa kushoto. 39#Zab 22:8; 109:25Nao waliokuwa wakipita njiani wakamtukana, wakitikisa-tikisa vichwa vyao, wakisema, 40#Mt 26:61; Yn 2:19Ewe mwenye kulivunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu, jiokoe nafsi yako; ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, shuka msalabani. 41Kadhalika na wale wakuu wa makuhani wakamdhihaki pamoja na waandishi na wazee, wakisema, Aliokoa wengine, hawezi kujiokoa mwenyewe. 42Yeye ni mfalme wa Israeli; na ashuke sasa msalabani, nasi tutamwamini. 43#Zab 22:9Amemtegemea Mungu; na amwokoe sasa, kama anamtaka; kwa maana alisema, Mimi ni Mwana wa Mungu. 44Pia wale wanyang’anyi waliosulibiwa pamoja naye walimshutumu vile vile.
Kifo cha Yesu
45Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hata saa tisa. 46#Zab 22:2Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? 47Na baadhi yao waliohudhuria, waliposikia, walisema, Huyu anamwita Eliya. 48#Zab 69:22Mara mmoja wao akaenda mbio, akatwaa sifongo, akaijaza siki, akaitia juu ya mwanzi, akamnywesha. 49Wale wengine wakasema, Acha; na tuone kama Eliya anakuja kumwokoa. 50Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake.
51 # Kut 26:31-33; Ebr 10:19,20 Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka; 52makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala; 53#Mdo 26:23; Dan 12:2nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi. 54Basi yule akida, na hao waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu, walipoliona tetemeko la nchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakisema, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu. 55#Lk 8:2-3Palikuwa na wanawake wengi pale wakitazama kwa mbali, hao ndio waliomfuata Yesu toka Galilaya, na kumtumikia. 56#Mt 20:20Miongoni mwao alikuwamo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo na Yusufu, na mama yao wana wa Zebedayo.
Kuzikwa kwa Yesu
57 # Mk 15:42-47; Lk 23:50-55; Yn 19:38-42 # Kut 34:25 Hata ilipokuwa jioni akafika mtu tajiri wa Arimathaya, jina lake Yusufu, naye mwenyewe alikuwa mwanafunzi wa Yesu; 58mtu huyu alimwendea Pilato akauomba mwili wa Yesu. Ndipo Pilato akaamuru apewe. 59Yusufu akautwaa mwili, akauzonga-zonga katika sanda ya kitani safi, 60#Isa 53:9akauweka katika kaburi lake jipya, alilokuwa amelichonga mwambani; akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda zake. 61Na pale walikuwapo Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, wameketi kulielekea kaburi.
Ulinzi katika Kaburi
62Hata siku ya pili, ndiyo iliyo baada ya Maandalio, wakuu wa makuhani, na Mafarisayo wakamkusanyikia Pilato, 63#Mt 16:21; 27:40; 12:40; 17:23; 20:19; Mk 8:31; 9:31; 10:33-34; Lk 9:22; 18:31-33wakasema, Bwana, tumekumbuka kwamba yule mjanja alisema, alipokuwa akali hai, Baada ya siku tatu nitafufuka. 64Basi amuru kwamba kaburi lilindwe salama hata siku ya tatu; wasije wanafunzi wake wakamwiba, na kuwaambia watu, Amefufuka katika wafu; na udanganyifu wa mwisho utapita ule wa kwanza. 65Pilato akawaambia, Mna askari; nendeni mkalilinde salama kadiri mjuavyo. 66#Dan 6:17Wakaenda, wakalilinda kaburi salama, kwa kulitia lile jiwe muhuri, pamoja na wale askari walinzi.

Iliyochaguliwa sasa

Mt 27: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia