Mit 13
13
1 #
1 Sam 2:25; Mit 9:7,8 Mwana mwenye hekima husikiliza mausia ya babaye;
Bali mwenye dharau hasikilizi maonyo.
2Mtu atakula mema kwa matunda ya kinywa chake;
Bali nafsi ya mtu haini itakula jeuri.
3 #
Zab 39:1
Yeye alindaye kinywa chake huilinda nafsi yake;
Bali afunuaye midomo yake atapata uharibifu.
4Nafsi ya mtu mvivu hutamani asipate kitu;
Bali nafsi ya mwenye bidii itanenepeshwa.
5 #
Kol 3:9; Rum 12:9 Mwenye haki huchukia kusema uongo;
Bali mtu mbaya huwa karaha, hupatwa na aibu.
6 #
Mit 11:3
Haki humlinda yeye aliye mnyofu katika njia yake;
Bali ubaya humwangusha mwenye dhambi.
7Kuna mtu mwenye kujitajirisha, lakini hana kitu;
Kuna ajifanyaye kuwa maskini, lakini ana mali nyingi.
8Dia ya nafsi ya mtu ni utajiri wake;
Bali mtu maskini hasikii ogofyo lo lote.
9Nuru ya mwenye haki yang’aa sana;
Bali taa ya mtu mbaya itazimika.
10Kiburi huleta mashindano tu;
Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana.
11 #
Mit 20:21
Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka;
Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa.
12Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua.
Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima.
13 #
2 Nya 36:16
Kila alidharauye neno hujiletea uharibifu;
Bali yeye aiogopaye amri atapewa thawabu.
14 #
Mit 16:22; 15:24; 2 Sam 22:6; Zab 116:3 Sheria ya mwenye akili ni chemchemi ya uzima,
Ili kuepukana na tanzi za mauti.
15Ufahamu mwema huleta upendeleo;
Bali njia ya haini huparuza.
16 #
Mit 12:23
Kila aliye na busara hutenda kazi kwa maarifa;
Bali mpumbavu hueneza upumbavu.
17Mjumbe mbaya huanguka maovuni;
Bali mjumbe mwaminifu ni afya.
18 #
Mit 15:5
Umaskini na fedheha zitampata yeye akataaye kurudiwa;
Bali yeye aangaliaye maonyo ataheshimiwa.
19Haja iliyopatikana ni tamu nafsini mwa mtu;
Bali kujitenga na maovu ni chukizo kwa wapumbavu.
20Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima;
Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.
21 #
Zab 32:10
Uovu huwaandamia wenye dhambi;
Bali mwenye haki atalipwa mema.
22 #
Mhu 2:26
Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi;
Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.
23 #
Mit 12:11
Chakula kingi chapatikana kwa ukulima wa maskini;
Bali viko viharibiwavyo kwa sababu ya dhuluma.
24 #
Mit 19:18; 22:15 Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe;
Bali yeye ampendaye humrudi mapema.
25Mwenye haki hula akaishibisha nafsi yake;
Bali tumbo la mtu mbaya litaona njaa.
Iliyochaguliwa sasa
Mit 13: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.