Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mit 14

14
1 # Rut 4:11; Mit 24:3,4 Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake;
Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.
2 # Ayu 12:4 Yeye aendaye kwa unyofu wake humcha BWANA;
Bali aliye mkaidi katika njia zake humdharau.
3 # Mit 12:6 Katika kinywa cha mpumbavu mna fimbo ya kiburi,
Bali midomo ya wenye hekima huwahifadhi.
4Zizi ni safi ambapo hapana ng’ombe;
Bali nguvu za ng’ombe zaleta faida nyingi.
5 # Kut 20:16 Shahidi mwaminifu hatasema uongo;
Bali shahidi wa uongo, pumzi zake ni uongo.
6 # Mit 17:24 Mwenye dharau hutafuta hekima, asiipate;
Bali maarifa huwa mepesi kwa mwenye ufahamu.
7Toka mbele ya uso wa mpumbavu,
Maana hutaona kwake midomo ya maarifa.
8 # Lk 12:20; 1 Kor 3:19 Akili za mwenye busara ni kujua njia yake;
Lakini upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu.
9 # Mit 1:22 Wapumbavu huidharau hatia;
Bali upo upendeleo kwa wenye haki.
10Moyo huujua uchungu wa nafsi yake,
Wala mgeni haishiriki furaha yake.
11 # Ayu 8:15; Mit 3:33 Nyumba ya mtu mbaya itabomolewa;
Bali hema ya mwenye haki itafanikiwa.
12 # Mit 16:25; Rum 6:21 Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu,
Lakini mwisho wake ni njia za mauti.
13 # Mhu 2:2 Hata wakati wa kucheka moyo huwa na huzuni;
Na mwisho wa furaha ni uzito wa moyo.
14 # Mit 12:14; 2 Kor 1:12; Flp 4:7 Ageukaye moyoni hushiba njia zake mwenyewe;
Na mtu mwema ataridhika nafsini mwake.
15Mjinga huamini kila neno;
Bali mwenye busara huangalia sana aendavyo.
16 # Mit 22:3 Mwenye hekima huogopa, akajitenga na uovu;
Bali mpumbavu ana ufidhuli, na kujitumai.
17Yeye aonaye hasira upesi atatenda kwa ujinga;
Na mtu mwenye hila mbaya huzirwa.
18Wajinga hurithi upumbavu;
Bali wenye busara huvikwa taji ya maarifa.
19Wabaya huinama mbele ya wema,
Na wasio haki malangoni mwao wenye haki.
20 # Mit 19:7 Maskini huchukiwa hata na jirani yake;
Bali tajiri ana rafiki wengi.
21 # Zab 41:1 Amdharauye mwenzake afanya dhambi;
Bali amhurumiaye maskini ana heri.
22Je! Hawakosi wawazao mabaya?
Bali fadhili na kweli zina wao wawazao mema.
23Katika kila kazi mna faida;
Bali maneno ya midomo huleta hasara tu.
24Taji ya wenye hekima ni mali zao;
Bali upumbavu wa wajinga ni upumbavu tu.
25Shahidi wa kweli huponya nafsi za watu;
Bali atoaye uongo hudanganya.
26Kumcha BWANA ni tumaini imara;
Watoto wake watakuwa na kimbilio.
27 # Mit 13:14 Kumcha BWANA ni chemchemi ya uzima,
Ili kuepukana na tanzi za mauti.
28Utukufu wa mfalme ni wingi wa watu wake;
Bali uchache wa watu ni uharibifu wa mkuu wao.
29 # Mit 15:18; Mt 11:29; 1 Kor 13:4,5; Yak 1:19 Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi;
Bali mwenye roho ya hamaki hutukuza upumbavu.
30 # Ayu 5:2; Zab 112:10; Mdo 7:9; Rum 1:29; Yak 4:5 Moyo ulio mzima ni uhai wa mwili;
Bali husuda ni ubovu wa mifupa.
31 # Ayu 31:15,16; Mhu 5:8; Mit 17:5; 22:2; Mt 25:40; 1 Yoh 3:17 Amwoneaye maskini humsuta Muumba wake;
Bali yeye awahurumiaye wahitaji humheshimu.
32 # Ayu 13:15; Zab 23:4; 2 Kor 1:9; 2 Tim 4:18 Mtu mbaya husukumwa chini katika kutenda mabaya kwake;
Bali mwenye haki ana matumaini katika kufa kwake.
33Hekima hukaa katika moyo wake mwenye ufahamu;
Bali yaliyo ndani ya wapumbavu hudhihirika.
34Haki huinua taifa;
Bali dhambi ni aibu ya watu wo wote.
35 # Mt 24:45-47 Upendeleo wa mfalme humwelekea mtumwa atendaye kwa busara;
Bali ghadhabu yake itakuwa juu yake aletaye aibu.

Iliyochaguliwa sasa

Mit 14: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia