Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mit 4

4
Ushauri wa Mzazi
1 # Zab 34:11; Mit 1:8 Wanangu, yasikilizeni mausia ya baba yenu,
Tegeni masikio mpate kujua ufahamu.
2Kwa kuwa nawapa mafundisho mazuri;
Msiiache sheria yangu.
3 # 2 Sam 12:24; 1 Nya 29:1 Maana nalikuwa mwana kwa baba yangu,
Mpole, mpenzi wa pekee wa mama yangu.
4 # 1 Nya 28:9; Efe 6:4 Naye akanifundisha, akaniambia,
Moyo wako uyahifadhi maneno yangu;
Shika amri zangu ukaishi.
5Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau;
Wala usiyakatae maneno ya kinywa changu.
6 # 2 The 2:10 Usimwache, naye atakuhifadhi;
Umpende, naye atakulinda.
7 # Mt 13:44; Lk 10:42 Bora hekima, basi jipatie hekima;
Naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu.
8 # 1 Sam 2:30; Dan 12:3 Umtukuze, naye atakukuza;
Atakupatia heshima, ukimkumbatia.
9Atakupa neema kuwa kilemba kichwani;
Na kukukirimia taji ya uzuri.
Maonyo kuhusu Kushika Njia ya Haki
10Mwanangu, sikiliza, na kuzipokea kauli zangu;
Na miaka ya maisha yako itakuwa mingi.
11Nimekufundisha katika njia ya hekima;
Nimekuongoza katika mapito ya unyofu.
12 # Zab 18:36; 91:11; Mit 3:23; 4:19; Yer 13:16; Yn 11:9,10 Uendapo, hatua zako hazitadhiikika,
Wala ukipiga mbio hutajikwaa.
13Mkamate sana elimu, usimwache aende zake;
Mshike, maana yeye ni uzima wako.
14Usiingie katika njia ya waovu,
Wala usitembee katika njia ya wabaya.
15Jiepushe nayo, usipite karibu nayo,
Igeukie mbali, ukaende zako.
16Maana hawalali isipokuwa wametenda madhara;
Huondolewa usingizi, ikiwa hawakumwangusha mtu.
17Maana wao hula mkate wa uovu,
Nao hunywa divai ya jeuri.
18 # Mt 5:14; Flp 2:15; 2 Sam 23:4 Bali njia ya wenye haki ni kama nuru ing’aayo,
Ikizidi kung’aa hata mchana mkamilifu.
19 # 1 Sam 2:9; Ayu 5:14; Isa 59:9,10; Yer 13:16; Yn 12:35 Njia ya waovu ni kama giza;
Hawajui ni kitu gani kiwakwazacho.
20Mwanangu, sikiliza maneno yangu;
Tega sikio lako, uzisikie kauli zangu.
21Zisiondoke machoni pako;
Uzihifadhi ndani ya moyo wako.
22Maana ni uhai kwa wale wazipatao,
Na afya ya mwili wao wote.
23Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo;
Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.
24Kinywa cha ukaidi ukitenge nawe,
Na midomo ya upotovu uiweke mbali nawe.
25Macho yako yatazame mbele,
Na kope zako zitazame mbele yako sawasawa.
26 # Ebr 12:13 Ulisawazishe pito la mguu wako,
Na njia zako zote zithibitike;
27 # Isa 1:16 Usigeuke kwa kuume wala kwa kushoto;
Ondoa mguu wako maovuni.

Iliyochaguliwa sasa

Mit 4: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia